Ndoto Zangu na Vikwazo Ninavyovipitia
Treasure Zakayo
Treasure Zakayo

Mimi ninaitwa Treasure. Mimi ninapenda kuwa mwalimu. Nina kipaji cha kusoma. Ninapenda kusoma vitabu vya hadithi kwa sababu vina maneno mazuri, michoro inayovutia, na vinaleta hisia mbalimbali kwa mfano huzuni, furaha, na masikitiko.

1

Pia ninapenda kusoma vitabu vya darasani, kwa mfano masomo ya Kiswahili na English.
Ninategemea kutumia kipaji changu kuwaelimisha watoto na kuwashauri kujiwekea ndoto zao.

2

Kuna watu wenye umuhimu kwangu ambao ni mama yangu, baba yangu, na walimu wangu. Wana umuhimu kwangu kwa sababu wananipa moyo wa kutokukata tamaa.

3

Ninasoma kwa bidii ili nifanikishe ndoto zangu. Ninajivunia kuwa mwalimu kwa sababu nitawaelimisha wanafunzi na kuwapa maarifa mema. Napenda jamii yenye michezo na ushirikiano.

4

Mdogo wangu alipozaliwa, kuna mbibi alikuja usiku kwenye kitanda ambacho mama na mdogo wangu wamelala. Alianza kuwanyonga. Iliacha alama kwangu kwa sababu kila nikifikiria naumia.

5

Nilipokuwa darasa la tano, baba yangu alinitumia fedha ya kununua kuku. Nilinunua kuku na kuanza kuwakuza. Japokuwa kuku wengine walikufa lakini sikukata tamaa, nikapambana nao na bibi alinisaidia kukuza.

6

Mpaka sasa hivi nina kuku wengi na tumegawana kuku na bibi. Nina furaha.
Ninamshukuru mungu kwa kunipa uhai. Ninamuomba mungu anipe kazi ya kuwa mwalimu.

7
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Ndoto Zangu na Vikwazo Ninavyovipitia
Author - Treasure Zakayo
Illustration - Treasure Zakayo
Language - Kiswahili
Level - First paragraphs