

Mimi ninaitwa Loveness. Mimi ni msichana. Ninapenda kuimba kwa sababu ndiyo kipaji changu na ninapenda kuimba ili kuendeleza kipaji changu. Watu wenye umuhimu kwangu ni wazazi walionizaa na walionilea kwa sababu wananifundisha maadili,
walimu walionitoa ujinga na kunipa maarifa, ndugu zangu kwa sababu wananipenda na wananijali, na makatekista na mapadre wangu kwa sababu wananifundisha sala na mambo ya kumtukuza Mungu.
Ninajivunia kuwa msichana kwa sababu msichana ni mwenye furaha, upendo, na uchangamfu kwenye kazi na vitu vingine. Mimi ninajivunia pale niliposoma kwa bidii na kufaulu. Nikawa wa kwanza kwenye mitihani yangu na nikapewa zawadi ya kufaulu.
Sehemu yenye umuhimu kwangu ni nyumbani kwa sababu nyumbani ninapata mahitaji yangu na haki zangu na pia kutimiza wajibu wangu. Kanisani ni sehemu muhimu kwangu kwa sababu ninapata kujua mambo yatupasayo kama kusali.
Shuleni ndiko mahali paliponitoa ujinga na kupata maarifa. Ndiyo sababu ni sehemu yenye umuhimu kwenye maisha yangu na ni historia ya maisha yangu. Shuleni ninapenda kufanya usafi wa mazingira na marafiki zangu.
Hospitali ni muhimu kwangu kwa sababu nina ndoto ya kuwa daktari na kutibu wagonjwa. Duka ni muhimu kwa ajili ya kununua bidhaa kama sukari, unga na mafuta. Bomba na mifereji ni muhimu kwa ajili ya kupata maji kwa sababu maji ni uhai.
Kitu kilichoacha alama kwenye maisha yangu ni rafiki yangu niliyempenda niliyemzoea katika kila shughuli alipoondoka na kukaa mbali na mimi. Niliumia na nililia aliponiacha. Ndio iliacha alama kwenye maisha yangu.
Ninamshukuru Mungu kwa zawadi aliyonipa ya kuwa na wazazi na ndugu wanaonipenda na wanaonithamini na pia hata zawadi ya wadogo zangu.

