

Ninaitwa Neema; Msichana ni anayeelimisha jamii na kufanya kazi kwa bidii. Ninajivunia kuwa msichana kwani ninaweza kusoma kwa bidii ili nifaulu. Ninataka dunia ijue wasichana wa Twiga wanaweza kusoma kwa bidii na kuwa wa kwanza Tanzania.
Ninaitwa Khyrati H; Msichana anaweza kuwa shujaa na mwalimu. Anaweza kufundisha jamii yake. Ninajivunia kuwa msichana kwakuwa nina nidhamu. Ninataka dunia iwachukulie wasichana wa Twiga kuwa ni wenye akili nyingi na nidhamu sana.
Zaituni; Msichana ni mchapakazi. Ninajivunia kuwa msichana kwakuwa nitatimiza malengo yangu ya kuwa raisi hapo baadae. Watu wanajua hatuwezi kufikia malengo, kumbe tunaweza kutimiza malengo yetu kama watu wengine mfano kutunza mazingira.
Naitwa Sania; Msichana ni mtu anayeweza kuwa msaada katika jamii yake mfano kuwa daktari wa kutibu watu au kuwa mwalimu wa kufunza watu. Ninajivunia kuwa msichana kwasababu msichana ana sifa nzuri sana mfano sifa ya usafi, adabu na nidhamu.
Jamii inapaswa kujua wasichana wa Twiga ni watulivu, wasikivu na wanyenyekevu. Ninataka dunia ijue wasichana wana umuhimu katika jamii kwani wana uwezo wa kuelimisha jamii kuhusu kilimo bora cha mbogamboga na jamii ikaelewa na kunufaika.
Naitwa Ashura; Msichana anaweza kuelimisha wanafunzi wenzake wakiwa darasani kwa kuwaambia wasipige kelele bali watulie wajisomee ili wafaulu masomo yao. Najivunia kuwa msichana kwasababu nina werevu mpana wa kuelimisha wanafunzi wenzangu.
Watu wanajua wasichana ni msaada wa baadae. Tunaweza kuelimisha jamii kuhusu kuacha matumizi ya dawa za kulevya na kutunza mazingira.
Nataka dunia ijue wasichana ni waelewa, wasikivu, na tunafanya kazi kwa usahihi na weledi mkubwa sana.
Ninaitwa Amina, Msichana ni msikivu anapoambiwa jambo. Wasichana hutunza mazingira kwa kupanda miti na maua.
Nataka dunia ijue wasichana wa Twiga ni wasafi na wanatunza mazingira kwa kupanda miti na maua.
Ninaitwa Jamila; Msichana ni mjasiriamali na mchapakazi.
Wasichana wa Twiga ni wachapakazi, watunza bustani, watunza mazingira na wanapenda kusoma kwa bidii ili kutimiza ndoto zao za baadae.
Naitwa Safi; Msichana ni anayeweza kusoma kwa bidii ili atimize ndoto zake za baadae kwa mfano kuwa daktari, nesi, injinia, mwalimu, mjasiriamali, mwenyekiti au kiongozi ili aweze kusaidia jamii yake. Ninajivunia kuwa msichana kwasababu,
msichana ni mnyenyekevu, jasiri na mwerevu. Msichana ni tegemezi la jamii sasa na baadae kwakuwa anaweza kusaidia watu wenye mahitaji na hata wasiojiweza. Wasichana ni wanaojituma na kufanya kazi kwa bidii sana.
Wasichana wanaweza kuwauguza wazazi wao pale wanapoumwa na wanaweza kufanya kazi za nyumbani bila shida yoyote.
Nataka dunia ijue wasichana wa Twiga ni wenye vipaji kama kuimba, kuchora, kuandika hadithi za maisha yao na wanapendana sana.
Ninaitwa Khayrat M; Msichana ni mchapakazi anayeweza kuelimisha jamii yake.
Ninajivunia kuwa msichana kwakuweza kuelimisha jamii usafi wa mazingira na afya zao.
Watu wanajua mimi ni lengo lao la baadae la kuokoa taifa.
Nitakuwa kiongozi wa baadae. Wazazi watajivunia kunileta shule. Nataka dunia ijue wasichana wa Twiga
wanaweza kusoma kwa bidii na kufikia malengo yao ya kuwa madaktari, wanasheria, marubani, walimu na wanajeshi ili kujenga taifa lao.
Ninaitwa Yusra; Msichana ni mwalimu katika jamii yake. Anaweza kuelimisha jamii yake
kuhusu haki ya msichana kuzungumza na kupata elimu ili atimize malengo yake.
Ninajivunia kuwa msichana kwakuwa ni tegemeo la baadae.
Ninaitwa Mwanamosi; Ninajivunia kuwa msichana kwakuwa ninapenda kujituma.
Watu wanajua mimi ni msikivu na mwelewa. Nilikuwa nina tabia ya kutupa taka ovyo,
nilipokatazwa niliiacha. Ninataka dunia ijue wasichana wa Twiga ni wasafi.
Ninaitwa Asma M; Msichana ni muelimisha jamii yake kama kushauri vitu na kufanya kazi kwa pamoja,
kuwasihi wasigombane na kulumbana. Ninajivunia kuwa msichana kwakuwa ninapenda jamii yangu.
Watu wanajua mimi ni kiongozi wao.
Ninaitwa Sumaiya; Msichana ni muelimisha jamii. Ninajivunia kuwa msichana kwa kuelimisha jamii.
Jamii ijue wasichana wa Twiga ni wanyenyekevu na wakarimu.
Ninataka dunia ijue wasichana wa Twiga ni wanyenyekevu na wasafi.
Naitwa Farhiya; Msichana ni mtunza mazingira na muelimisha jamii ipande miti na kufanya usafi. Najivunia kuwa msichana kwa kutunza mazingira na kusaidia jamii kuepuka magonjwa. Nataka dunia ijue wasichana wa Twiga ni watunza mazingira.
Ninaitwa Rujaina M; Msichana anaweza kuelimisha jamii na kufanya shughuli kama kufua.
Ninajivunia kuwa msichana kwani ninaweza kusoma kutimiza ndoto yangu ya uandishi wa habari.
Jamii inajua wasichana hawawezi kujifunza.
Ninaitwa Asma S; Msichana ni mjasiri anaweza kuvumilia jambo.
Jamii inajua wasichana wa Twiga ni wachapakazi na hufanya kazi kwa bidii.
Nataka dunia ijue wasichana wa Twiga ni mfano wa kuigwa na shule zote zinazotuzunguka.
Naitwa Rujaina R; Msichana ni mwerevu na msikivu, akiambiwa jambo analitekeleza. Najivunia kuwa msichana kwakuwa ninategemewa na jamii na familia yangu. Nataka dunia ijue wasichana wa Twiga ni werevu, wasikivu na wenye upendo kwa jamii yao.
Naitwa Nurath; Msichana husaidia watu wasiojiweza kama watoto yatima.
Ninajivunia kuwa msichana kwakuwa msichana
ni mchapakazi anayelinda nchi yake na kusaidia wazazi wake.
Jamii inajua wasichana ni watetea wanyonge.
Paskalia; Msichana ni ambaye anajituma kwa bidii afanikishe ndoto zake za baadae. Msichana anaweza kila jambo na husaidia ndugu zake. Ninataka dunia iwachukulie wasichana wanaweza kufanya kazi yoyote bila kuambiwa na kuifanya vizuri.
Naitwa Nairat; Msichana ni mchapakazi na hujali wengine. Msichana ni mzalendo na husaidia kazi.
Nataka dunia ijue wasichana wa Twiga ni wachapakazi, wacheza mpira wa miguu,
netball, ngumi, rede na wengine ni mashabiki.
Samia; Msichana ni mchapakazi. Najivunia kuwa msichana ili kutimiza ndoto zangu za udaktari au mwalimu. Watu wanajua wasichana ni wacheshi, wapambania nchi na watoa msaada. Nataka dunia ijue wasichana ni wachapakazi, wacheshi na wapambanaji
Ninaitwa Josefina; Msichana hushirikiana na wenzake. Ninajivunia kuwa msichana kwakuwa
ninaweza kushirikiana na wenzangu. Wasichana hujituma na hupenda kufanya kazi.
Ninataka dunia ijue wasichana wa Twiga ni wachapakazi.
Naitwa Rukia; Ninajivunia kuwa msichana kwa kuweza kufanya kazi shuleni na nyumbani.
Msichana ni mzalendo kwa kusaidia yatima, walemavu na vipofu.
Ninataka dunia ijue wasichana wa Twiga wanafanya kazi kwa bidii.
Naitwa Aisha; Msichana ni mjasiriamali. Najivunia kuwa msichana kwasababu ninajua kuchora.
Watu wanajua wasichana ni muhimu na huwapenda.
Nataka dunia ijue wasichana ni wazuri, tunajivunia na kujipenda.
Swaumu; Msichana hufanya kazi mbalimbali kama vile kuosha vyombo, kupika na kudeki. Najivunia kuwa msichana kwani ni shupavu na mpambanaji. Nataka dunia ijue wasichana wa Twiga wana sifa nzuri na wanapenda wanafunzi wenzao na walimu wao.

