

Ninaitwa Yusra Mohammed, ninaamini kuwa msichana ni mwalimu katika jamii yake,anaweza kuelimisha jamii yake kuhusu haki ya msichana kuzungumza na kupata elimu ili atimize malengo yake.Ninajivunia kuwa msichana Kwa kuwa ni tegemeo la baadae.
Ninaitwa Amina Omari ,msichana ni msikivu anapoambiwa jambo.Watu huwachukulia wasichana kama watunza mazingira kwa kupanda miti na maua.Nataka dunia iwachukulie wasichana wa Twiga ni wasafi na watunza mazingira kwa kupanda miti na maua.
Ninaitwa Jamila Saidi,msichana ni mjasiriamali na mchapa kazi.Watu wanawachukulia wasichana wa Twiga kama ni wachapakazi,watunza bustani,watunza vyanzo vya maji ,watunza mazingira yao na wanapenda kusoma kwa bidii kutimiza ndoto za baadae.
Naitwa Neema Michael,msichana ni anaye elimisha jamii na kufanya kazi Kwa bidii.Ninajivunia kuwa msichana kwani ninaweza kusoma kwa bidii ili nifaulu.Nataka dunia ijue wasichana wa Twiga wanaweza kusoma kwa bidii na kuwa wa Kwanza Tanzania.
Ninaitwa Khyrati M,msichana ni mchapakazi anayeweza kusaidia jamii yake kwa kuwaelimisha,Ninajivunia kuwa msichana kwa kuweza kuelimisha jamii usafi wa mazingira na afya zao.Watu wananichukulia kuwa lengo lao la baadae kuokoa taifa.
Nitakuwa kiongozi,wazazi nao watajivunia kunileta shule.Ninataka dunia ijue wasichana wa Twiga wanaweza kusoma kwa bidii na kufikia malengo yao ya kuwa madaktari,wanasheria,marubani, walimu au wanajeshi ili kujenga taifa lao la Tanzania.
Ninaitwa Safi,msichana ni mtu anayeweza kusoma kwa bidii ili atimize ndoto zake za baadae Kwa mfano kuwa daktari,nesi,injinia,mwalimu,mjasiriamali,mwenyekiti au kiongozi ili aweze kusaidia jamii yake.Ninajivunia kuwa msichana kwa sababu,
msichana ni mnyenyekevu,mkakamavu,mjasiri na mwerevu.Msichana ni tegemezi la jamii sasa na baadae kwakuwa anaweza kuwasaidia watu wenye mahitaji na hata wasiojiweza.Watu wanawachukulia wasichana ni watu wanaojituma na kusoma kwa bidii sana.
Wasichana wanaweza kuwauguza wazazi wao pale wanapoumwa na wanaweza kufanya kazi za nyumbani bila shida yoyote.Nataka dunia ijue wasichana wa Twiga ni wenye vipaji kama kuimba,kuchora, kuandika hadithi za maisha yao na wanapendana Sana.
Ninaitwa Rujaina M,msichana anaweza kuelimisha jamii na kufanya shughuli kama vile kufua.Ninajivunia kuwa msichana kwani ninaweza kusoma kutimiza ndoto yangu ya uandishi wa habari.Jamii inachukulia wasichana ni wadogo hawawezi kujifunza.
Ninaitwa Khyrati H, msichana anaweza kuwa shujaa na mwalimu.Anaweza kufundisha jamii yake.Ninajivunia kuwa msichana Kwa kuwa nina nidhamu.Nataka dunia iwachukulie wasichana wa Twiga kuwa ni wenye akili nyingi na nidhamu sana.
Lujayna R,msichana ni mwerevu na msikivu,akiambiwa kitu anakitekeleza.Ninajivunia kuwa msichana Kwa kuwa nategemewa na jamii na familia yangu.Nataka dunia iwachukulie wasichana wa Twiga ni werevu ,wasikivu na wenye upendo juu ya jamii.
Sumaiya,msichana ni mtu anayeweza kuelimisha jamii.Ninajivunia kuwa msichana kwa kuelimisha jamii.Jamii iwachukulie wasichana wa Twiga ni wanyenyekevu na wakarimu.Dunia iwachukulie wasichana wa Twiga ni wakarimu,wanyenyekevu na wasafi sana
Asma S,msichana ni mjasiri anaweza kuvumilia jambo.Jamii inachukulia wasichana wa Twiga ni wachapakazi.Nataka dunia ijue wasichana ni wachapakazi na hufanya kazi kwa bidii.Wasichana wa Twiga ni mfano wa kuigwa na shule zote zinazotuzunguka.
Zaituni,msichana ni mchapakazi.Najivunia kuwa msichana kwakuwa nitatimiza malengo yangu ya kuwa raisi hapo baadae.Watu hutuchukulia kama hatuwezi kufikia malengo,kumbe tunaweza kutimiza malengo yetu kama watu wengine kama kutunza mazingira.
Josephina,msichana ana uwezo wa kushirikiana na wenzake.Ninajivunia kuwa msichana kwakuwa ninaweza kushirikiana na wenzangu.Watu hutuchukulia wasichana tunajituma na tunapenda kufanya kazi.Nataka dunia ijue wasichana wa Twiga ni wachapakazi
Samia,msichana ni mchapakazi,najivunia kuwa msichana ili kutimiza ndoto zangu za udaktari au mwalimu.Watu wanawachukulia wasichana ni wacheshi,wapambania nchi yao na watoa misaada.Dunia ijue wasichana ni wachapakazi,wacheshi na wapambanaji.
Swaumu,msichana hufanya kazi mbalimbali kama vile kuosha vyombo,kupika na kupiga deki.Najivunia kuwa msichana kwasababu ni shupavu na mpambanaji.Dunia ichukulie wasichana wa Twiga wana sifa nzuri na wanapenda wanafunzi wenzao na walimu wao.
Nairat,msichana ni mchapakazi na hujali wengine.Watu wananichukulia mzalendo kwa kusaidia kazi.Dunia ituchukulie wasichana wa Twiga ni wachapakazi,wacheza mpira wa miguu, wacheza netball,wacheza ngumi,wacheza rede na wengine ni mashabiki.
Aisha, msichana ni mjasiriamali. Najivunia kuwa msichana kwasababu najua kuchora. Watu wanachukulia wasichana ni muhimu na huwapenda.Nataka dunia ituchukulie wasichana ni wazuri,tunajivunia na kujipenda.
Farhiya,msichana ni mwenye uwezo wa kutunza mazingira,kuelimisha watu wapande miti na kufanya usafi.Ninajivunia kuwa msichana kwa kutunza mazingira yangu vizuri na kusaidia jamii kuepuka magonjwa.Dunia ijue wasichana ni watunza mazingira.
Rukia,msichana hujivunia kuwa msichana,najivunia kuwa msichana kwa kuweza kufanya kazi za shuleni na nyumbani.Watu wananichukulia kama mzalendo kwa kusaidia yatima,walemavu,na vipofu.Nataka watu watuchukulie kama wafanya kazi kwa wa bidii.
Ashura,msichana anaweza kuelimisha wanafunzi wenzake wakiwa darasani,kwakuwaambia wasipige kelele bali watulie na wajisomee ili wafaulu masomo yao.Najivunia kuwa msichana kwasababu nina werevu mpana wa kuweza kuelimisha wanafunzi wenzangu.
Watu hutuchukulia wasichana kama msaada wa baadae, kwani tunaweza kuelimisha jamii kuhusu kuacha dawa za kulevya na kutunza mazingira.Nataka dunia ielewe wasichana ni waelewa,wasikivu na tunafanya kazi Kwa usahihi na weledi mkubwa sana.
Naitwa Nurath,msichana ni mtu anayesaidia watu wasiojiweza kama kukaa na watoto yatima. Ninajivunia kuwa msichana kwakuwa msichana ni mchapakazi anayelinda nchi yake na kusaidia wazazi wake.Jamii inachukulia wasichana ni watetea wanyonge.
Paskalia,msichana ni mtu ambaye anajituma kwa bidii afanikishe ndoto yake ya baadae.Msichana anaweza kila jambo na kusaidia ndugu zake.Ninataka dunia iwachukulie wasichana wanaweza kufanya kazi yoyote bila kuambiwa na kufanya kazi vizuri.
Ninaitwa Sania,msichana ni mtu anayeweza kuwa msaada katika jamii yake mfano kuwa daktari wa kutibu watu au kuwa mwalimu wa kufunza watu.Ninajivunia kuwa msichana kwasababu msichana ana sifa nzuri sana mfano sifa ya usafi, adabu na nidhamu.
Jamii inapaswa kujua wasichana wa Twiga ni watulivu, wasikivu na wanyenyekevu.Ninataka dunia ijue wasichana wana umuhimu katika jamii kwani wana uwezo wa kuelimisha jamii kuhusu kilimo bora cha mboga mboga na jamii ikaelewa na kunufaika.
Ninaitwa Mwanamosi, ninajivunia kuwa msichana kwakuwa ninapenda kujituma.Watu wananichukulia kama msikivu na mwelewa,nilikuwa nina tabia ya kutupa taka ovyo, nilipokatazwa niliiacha.Ninataka dunia ijue wasichana wa Twiga ni wasafi.
Ninaitwa Asma M, msichana ni mtu anayeweza kuelimisha jamii yake kama kushauri vitu na kufanya kazi kwa pamoja, kuwasihi wasigombane na kulumbana.Najivunia kuwa msichana kwakuwa ninapenda jamii yangu.Watu wananichukulia kama kiongozi wao.

