

Mimi ninaitwa Sayuni. Ninasoma Shule ya Msingi Ngarash. Nina miaka kumi na moja.
Nina kipaji cha kuchora. Pia ninapenda kusoma hadithi za kishujaa.
Nina ndoto ya kuwa daktari. Mimi ninapenda kucheza kwa sababu kucheza ni moja ya aina ya mazoezi ya kuimarisha mwili. Na pia husaidia kunilinda dhidi ya magonjwa mbalimbali mfano kisukari na mengineyo mengi.
Watu wenye umuhimu kwenye maisha yangu ni marafiki, wazazi, na watu walionizidi umri. Umuhimu wa kwanza tuanze na rafiki. Niliwahi kuanguka. Rafiki yangu Loveness alienda kutoa taarifa kwa mwalimu. Akaweza kunifikisha zahanati.
Nilipopona nilimshukuru sana. Kuanzia siku hiyo tunasaidiana kwa kila kitu mithili ya ndugu. Nikiwa na upweke ananifariji. Umuhimu wa wazazi husaidia kutununulia uniform za shule.
Shuleni ndiyo sehemu yenye umuhimu kwangu. Hutoa elimu na kunifikisha viwango vya juu na kunifanya nitimize ndoto zangu na vipaji vyangu.
Mimi najivunia kuwa msichana kwa sababu msichana ni mtu mwenye upendo mwingi na huvumilia vitu vingi. Na msichana anastahili kupendwa.

