

Sisi ni wasichana wa darasa la 5 na la 6 kutoka Shule ya Msingi ya Mwasi Kaskazini, mkoani Kilimanjaro. Tumeandaa kitabu hiki katika klabu yetu ya Hadithi Zetu mwaka 2025.
Tunaamini kwamba msichana ni mtu wa kipekee. Soma kitabu hiki ujifunze umuhimu wetu sisi wasichana kwenye jamii!
Ninaitwa Sofia. Ninajivunia kuwa msichana kwa sababu ninaweza kutetea haki za wasichana. Niliweza kutetea haki ya msichana mwenzangu wakati babake alimwambia hakuna kwenda shule ili awe yaya wa kubeba mdogo wake.
Watu wanachukulia wasichana ni wa
kubeba watoto au kufanya kazi za nyumbani. Hawataki kuwapeleka shule. Kwa mfano, dada alikuwa amefika darasa la 4. Baba alimwambia, "Hakuna kurudia darasa la 4." Dada alijitetea, "Nitarudia kwa ajili ya elimu nitakayoipata shuleni." Baba alimwambia,
"Nenda kaolewe tu." Dada alisema, "Nitakushitaki." Baba alimchapa na dada alikimbia na kwenda kwa mjomba wa babake. Yuko huko mpaka leo. Anataka tena kurudi nyumbani kwa sababu hawataki kumnunulia nguo ya sikukuu. Sasa anafanya kazi kwa watu. Hiyo sio haki.
Ninaitwa Onesma. Msichana ni jasiri, mstahimilivu, na mwenye unyenyekevu na utu. Msichana anaheshimu watu na jamii inayomzunguka.
Ninajivunia kuwa msichana kwa sababu sina ukorofi wala sina matukano, dharau, au wizi.
Mimi ninataka dunia ijue kuwa wasichana
wa Mwasi ni wachapakazi kama darasa la 6 na la 5 tulivyoungana tukajenga kitu chetu kinachoitwa klabu. Klabu yetu ni nzuri.
Ninataka mpaka nchi za nje zijue kuwa wasichana wa Mwasi ni wachapakazi kwa sababu tunapiga kazi bila kulazimishwa au kuambiwa.
Mimi ninaitwa Eliza. Ninajivunia kuwa msichana kwa sababu mimi ni mtu jasiri, mwenye nguvu, na mwenye kujua kudai haki yangu. Mimi nitadai haki yangu ya kusikilizwa.
Msichana sio mtu wa kumwozesha mapema. Wasichana wasome mpaka wakitaka kuolewa wakubali wenyewe.
Pia msichana anajua lugha nyingi. Anatakiwa kuthaminiwa ili aweze kufikia ndoto zake za baadaye. Kwa mfano, msichana ana ndoto ya kuwa rubani, mwalimu, mwanasheria, na daktari.
Wasichana wafoi wakundi kwenda kusoma. Msichana ni mtu mwenye akili, mwenye maarifa,
sio msichana kwenda kuchota mringa wakati mtu mwingine amekaa nyumbani. Hiyo siyo haki, kwonyisuo?
Wandu wanatesa na kuwabagua wasichana kama vile wababa wachache wanaoendelea na desturi za zamani.
Tunaomba mzire owinyi, tumeelewana mwonyisuo?
Ninaitwa Tunu. Msichana anapenda sana watu. Akimwona mtoto anaanguka anamdaka. Msichana hakati tamaa katika magumu anayokutana nayo. Anajua kuvumilia katika shida na raha. Wasichana wengi hupenda sana masomo na wanajua kulilia haki zao kwa sababu hulilia sana kwenda shuleni.
Wasichana wafoi wakundani sana wakati wingi nakeri shuleni, kanisani, nyumbani. Ngi kiki ngaamba kuro? Ko sababu le kama nguo yajikunja na kemfumulia necha njikundi sana wasichana.
Wasichana le njiwakundi ko sababu le wakundi kasi ndogondogo wakundi jishuhulisha mno.
Ninaitwa Francisca. Msichana ni mwenye nguvu na upendo. Msichana ni mvumilivu na ni mtu anayefaulu mitihani yake. Najivunia kuwa msichana kwa sababu nafanya kazi kwa pamoja. Najivunia kuvaa sketi, suruali, na magauni.
Wanaona msichana ni mtu mwenye mahari tu.
Wanawabagua. Wasichana wanakeketwa na kutopewa haki za msingi wanazohitaji. Wasichana wasibaguliwe wasikeketwe. Wasichana wanataka kupewa elimu.
Kwenye mchoro, msichana anaangalia bustani yenye migomba na miti. Wanafunzi wanaruka kamba kwa ushirikiano.
Ninaitwa Marta. Msichana ni mwenye utu, upendo, na uvumilivu. Msichana ni mchapakazi. Hupenda kusoma kwa bidii katika masomo yote.
Waache wasichana wawe na uhuru wa maisha yao na kufikia malengo yao, kwa mfano ya kuwa mwalimu kufundisha watu katika jamii ya Mwasi Kaskazini.
Ninaitwa Edith. Msichana husaidiana katika masomo, michezo, kutunga vitabu, na kuchora picha. Msichana huwasaidia wenye shida, kama wasiojua kusoma na kuandika.
Ninajivunia kuwa msichana kwa sababu nina upendo na ushirikiano katika kuwasaidia wagonjwa, michezo, na kusoma pamoja.
Ninaitwa Anna. Najivunia kuwa msichana kwa sababu msichana anasaidia wenzake kwa upendo. Kwa mfano, mwenzake darasani akikosea au hawezi kufanya maswali, atamsaidia kwa kumwelewesha. Kama mwenzake hana peni, anamsaidia moja.
Msichana anajituma kulima na kufuga ng'ombe na kuku.
Msichana ni mwenye ujasiri kwa sababu anaweza kuongea mbele ya maelfu ya watu.
Msichana habagui wenzake, awe kilema au mzima. Wamwache mwenzao darasani kwa kuwa yeye ni kilema halafu wao waende kucheza, hapana. Hivyo haitakiwi. Wanatakiwa wote wacheze pamoja.

