NDOTO YANGU
Fatma Maleta
Vusi Malindi

Ilikuwa asubuhi na mapema,jua lilikuwa limeshachomoza niliamka nikiwa nimechoka sana.

1

Pembeni yangu alikuwepo mdogo wangu Mkwai ambaye alikuwa akinguruma kama Simba.
Mkwai aliliala fofofo.

2

Sikumuamsha kwanza,hivyo niliendelea kutandika kitanda.Mara pap! mama akaita "Mkwai, Mkwai amka tena haraka, amka ujiandae uende shule."
Mkwai aliamka amekasirika sana."Daa ,kila siku shule tu."
Mkwai ntakupiga asubuhi hii we nitafute tu.

3

Baada ya hapo niliweka maji yangu kwenye beseni nikaanza kusafisha uso na kinywa changu.

4

Niliendelea kupiga mswaki taratibu huku mama akinisimamia Kwa makini sana.

5

Kisha nikaanza kuoga huku nikijisugua taratibu.Nilijisugua huku na kule nikiimba
Mtama, mtamu,
Mta,mta,mtamuuuuuu.

Wimbo ulik

6

Mama alinisaidia kuvaa nguo zangu za shule kisha akaniambia"Mwanangu Zai u some Kwa bidii, uje uwe na maisha unaniona mimi mama yako navopata tabu, ningekuwa nimesoma , ningekuwa mbali zaidi kimaisha na kifikra.

7

Sawa mama nilijibu .Mkwai nae alikuwa tayari kashajiandaa tukaongozana wote shuleni.Wakati tupo njiani, nilimuuliza mdogo wangu, "Mkwai , wewe ukiwa mkubwa, ndoto yako ni kuwa nani?"

8

Eiiiii........Mimi Nataka kuwa Pacome si unaona staili zangu za mipira Yani nikipiga shuti linaruka huko mbiguni , linarudi.Mmhh ni ndoto nzuri sana , Mimi napenda udaktari .Vizuri.
Mkwai tuwahi nina somo la hesabu na Mwalimu Yahya asubuhi

9

Asubuhi chupuchupu nikose lile somo .Wakati wa mapumziko tulicheza mpira na Pacome mtarajiwa Yani Mkwai alifungwa magoli mengi ,akabadili ndoto yake ,"Mmh au nitakuwa screen protector wa yanga nikishindwa naenda Simba .Haah....tulicheka.

10

Mpira ulipoisha nilivaa viatu na watoto wote tukaelekea nyumbani.Mkwai Leo wamejua kukufunga Hadi umeamua kuwa Kipa .Ni ndoto yangu, ndoto yangu we niache baki na yako.
Sawa ,sawa.Mimi na Mkwai tuna ndoto zetu.

Je wewe ndoto yako ni nini?

11
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
NDOTO YANGU
Author - Fatma Maleta
Illustration - Vusi Malindi
Language - Kiswahili
Level - First paragraphs