

Tanzania ni nchi iliyopo barani Afrika na inajulikana kwa vivutio mbalimbali vinavyopatikana ndani yake. Lugha kuu ya mawasiliano inayotumika ni lugha ya Kiswahili. Pia Tanzania inasifika kuwa na makabila mengi zaidi ya 120 mf:wachaga, n.k.
Licha ya kuwa na makabila mengi pia Tanzania ni nchi yenye amani na furaha.
Tanzania ni nchi yenye vivutio vingi vya kushangaza na kupendeza. Vivutio hivyo vinahusisha hifadhi za wanyama, mito, fukwe za bahari n.k.
Pia Tanzania imebarikiwa kuwa na aina mbalimbali za madini mfano almasi, dhahabu, bati na tanzanite ambayo hupatikana Tanzania pekee.
URITHI WA TANZANIA
Urithi unajumuisha vitu vyenye thamani na kumbukumbu zilizo hifadhiwa au kuwepo katika eneo fulani kutoka vizazi vilivyopita. Urithi huu unaweza kuwa unaoshikika au usioshikika.
Urithi unaoshikika unahusisha majengo, vyanzo vya maji, misitu, na miundombinu. Urithi usioshikika unahusisha amani, utawala bora na misemo yenye kujenga jamii.
Mkoa wa Arusha uliopo Tanzania kuligundulika fuvu la Kwanza la binadamu wa kale na dokta Louis Leakey na mkewe Mary Leakey mwaka 1959
Michoro ya kale iliyopo kondoa irangi mkoani Dodoma. Michoro hiyo inaelezea maisha walioishi binadamu wa kale ambao ni mababu zetu. Michoro hii inaelezea mgawanyo wa kazi kwa vijana wa kike na vijana wa kiume
SANAA ZA JADI
Sanaa za jadi ni zile kazi zinazofanywa na wanajamii wa Jamii fulani. Mfano wa Sanaa hizi ni Ngoma za asili, uchongaji, ususi wa mikeka na vikapu, ufinyanzi wa vyungu n.k
JUKUMU LETU
Sisi kama watanzania inatupasa kutunza hazina hizi na vivutio tulivyo rithishwa na mababu zetu. Na kuhamasisha utunzaji wa mazingira na kuenzi mila na desturi zetu

