Ndoto Zetu
Wanafunzi wa Maktaba ya Jamii Cheche
Wanafunzi Wa Maktaba ya Jamii Cheche

Ninaitwa Esther. Ndoto yangu ni kuwa mwalimu ili nielimishe wanafunzi na watimize ndoto zao. Nitawaelimisha watoto wasome ili wafikie malengo yao. Pia nitaelimisha jamii yangu ipambane na rushwa ili rushwa iishe. Ninataka jamii yangu iwe na maadili na uangalifu mkubwa.

1

Ninataka nisome hadi chuo kikuu cha ualimu kwa sababu watu wengi katika familia yangu walikuwa walimu, kwa mfano bibi zangu, babu, baba yake bibi, na mjomba. Nilipoona hivyo na mimi nikataka kuwa mwalimu.

Ninapenda kujua lugha za Kinyiramba, Kinyaturu, na Kichaga.

2

Ningependa jamii yangu iwe imedhibiti vitendo visivyo vya maadili ili tuishi kwa amani.

Ninapenda kuishi Dodoma kwa sababu nimependa mazingira ya kule. Na pia ningeweza kwenda kuangalia mashamba ya bibi zangu kirahisi maana Dodoma ni karibu na Singida.

3

Ninapenda jamii yangu. Ninataka nikiwa mkubwa nisaidie maskini na wasiojiweza.

Nataka kuwa na familia yenye maadili na utaratibu. Na nataka niwe na watoto zaidi ya watatu.

Nina uwezo wa kusikiliza jamii yangu na kuisaidia.

4

My name is Josephina. Ndoto yangu ni kuwa mwanajeshi kwa sababu nataka kutetea jamii yangu na kuilinda. Ninataka kufanya kazi katika jeshi la kulinda nchi.
Mimi nataka kusoma mpaka chuo kikuu. Nitasoma kwa bidii ili kutimiza ndoto zangu.

5

Nataka kuongea Kiingereza, Kiswahili, Kimaasai, Kifaransa, na Kichina ili kutimiza ndoto zangu. Nitawafundisha watu ambao hawazifahamu lugha hizi.

Nataka kuwa na familia yenye furaha na amani. Pia nataka kuwa na mtoto mmoja kwenye maisha yangu.

6

Nina ndoto ya kuwasaidia watoto yatima katika jamii ili wafikie ndoto zao. Nitawasaidia kwa kuwapa mahitaji mbalimbali, kwa mfano chakula, nguo, na kuwasaidia katika masomo ambayo hawayafahamu.

Nataka kuwa na jamii yenye ushirikiano na upendo.

7

Mimi nataka kuishi Monduli kwa sababu nimezaliwa Monduli na napapenda.

Nitaelimisha jamii kwamba kila mtoto ana haki ya kusoma kwa sababu wote binadamu.

I want to be a soldier. I love my dreams.

8

Mimi ninaitwa Kelvin Yona. Mimi nina ndoto ya kuwa mchoraji. Ninatamani baadaye niwe mchoraji mkubwa. Ninataka kuwa naendesha magari na pikipiki. Pia ninataka kuwapa wanajamii elimu mbalimbali.
Mimi ninataka kuishi Arusha kwa sababu kuna ndugu zangu.

9

Malengo yangu ni kuwa mchoraji na niwajengee wazazi wangu ghorafa kubwa.

Ninataka kusoma mpaka chuo kikuu. Ninataka kuwa na familia yenye amani na ninataka kuwa na watoto wawili. Nina ndoto kwa wanajamii wakuze ndoto zao. Ninataka jamii initie moyo wasinikatishe tamaa.

10

Ninataka kuongea Kiingereza na Kifaransa kwa sababu unaweza kwenda nchi za mbali kama vile Ufaransa na Burundi, na lugha hizo zinaweza kukusaidia kuelewana na watu mbalimbali.

Mimi pia ninapenda kuwa mchoraji kwa sababu fani yangu ni kuchora vizuri.

11

Nitakuwa mtu maarufu na mwenye ujuzi. Pia mimi ninapenda kuchora kwenye ukuta wa mashuleni na kompasheni mbalimbali kwa ajili ya kuwafurahisha watoto na hata watu wakubwa.
Nataka niwe nawasaidia watu wengi na jamii iwe na amani na upendo.

12

Mimi ninaitwa Leonard. Nina ndoto ya kuwa mchezaji mpira. Ninapenda nikiwa mkubwa niwe mchezaji na niwe dokta niwatibu wagonjwa ili wasipatwe na magonjwa kwa maana kuna watu wanaumwa na magonjwa mbalimbali.
Ninataka kusoma mpaka chuo kikuu.

13

Ninataka kuleta mabadiliko kwa jamii yangu. Ninataka kuwajengea wanajamii maghorofa, kuwajengea uwanja wa mpira kama uwanja wa Sabasaba, na kuwajengea viwanda vya matofali na viatu na mabomba ya maji. Nitawapa ajira mbalimbali kama uuzaji wa mandazi, ndizi, na maembe.

14

Nitawasisitiza wazazi wawapeleke watoto shuleni na wazazi kupata kipato ili waweze kulima na kufuga.

Nitawasaidia wazazi wangu na kuwajengea nyumba kubwa ya kifahari yenye vitu mbalimbali kama kitanda, meza, viti na mimea mbalimbali kama machungwa, mafenesi, na mazambarau.

15

Ninataka kuwa na familia nzuri na kuwa na watoto 2.

Ninahitaji kujua lugha za Kiswahili, Kiingereza, Kimaasai, Kichina, Kifaransa, Kituruki, na Kifilipino.

Ninataka kuishi Monduli kwa sababu Monduli ina maji, mabomba, na uwanja wa mpira.

16

Mimi ninaitwa Winfrida. Nikiwa mkubwa ninataka kuwa mwalimu ili niwafundishe wanafunzi na wafaulu mitihani yao.

Ninataka wazazi wapendane, na watu kwenye jamii yangu wapendane. Nitaishi Arusha. Nataka kuwa na mtoto mmoja.

17

Nataka niongee Kiswahili, English, na Kichaga. Niwafundishe jamii na wazazi wangu lugha hizo.

Nataka kusoma hadi chuo kikuu, somo la sayansi. Nataka niwe na jamii ya wasomi. Nataka niwe mchezaji bora wa kucheza rede, mpira, na michezo mbalimbali.

18

Ndoto yangu ni kusaidia wanajamii na kuwasaidia watu wengi wafanye kazi kwa bidii kwa kusaidiana. Nitawasaidia kufanya kazi mbalimbali kama vile kulima, kuotesha bustanini, kuotesha mbogamboga na matunda, kuotesha miti na vitu mbalimbali kama maua.

19

Ndoto yangu ni kuwa mwalimu. Nitasimamia usafi wa mazingira ili mazingira yawe safi.

Nina ndoto ya wanajamii wangu wapendane wasaidiane kazi mbalimbali. Ninapenda sana kusoma kwa bidii ili nisaidie jamii yangu.

20

Mimi naitwa Ismaili. Ndoto yangu ni kuwa Daktari. Natamani baadaye niwe daktari mzuri wa kusaidia watu kama wazee, vijana na watoto kwa sababu lazima watu wapate huduma. Wasipopata huduma watapoteza maisha. Maisha ya watu ni muhimu. Nataka kuokoa maisha ya watu.

21

Mimi naitwa Maiko. Nitakapokuwa mkubwa nitakuwa mwalimu na rubani kwa ajili ya kuimarisha taifa halafu kuwasaidia wazazi wangu na kuwasaidia wanafunzi maisha ya baadaye kuwa mazuri. Nataka kuwa mwalimu ili kuwasaidia wanafunzi malengo ya baadaye.

22

Pia nitaimarisha jamii na nchi na kulijenga taifa letu ili kupata fedha ya kuwasaidia wanajamii. Nataka jamii yangu iwe na furaha tele. Nataka kuwa na jamii ya wasomi.

Nitakapokuwa mkubwa nitakuwa Mfaransa, Mmeru, na Mmaasai.

23

Nitakuwa na watoto 9. Nataka kuwa na familia yenye furaha na amani. Familia yangu ipende kanisa na kumwabudu mungu. Watoto wangu wasome kwa bidii na wasipende kununa. Nataka kusoma hadi chuo kikuu.

Nahitaji kuwa na lugha 3: Kifaransa, Kimeru, na Kimaasai.

24
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Ndoto Zetu
Author - Wanafunzi wa Maktaba ya Jamii Cheche
Illustration - Wanafunzi Wa Maktaba ya Jamii Cheche, Maktaba Ya Jamii Cheche
Language - Kiswahili
Level - First paragraphs