Ndoto Zangu za Baadaye
Emmanuel Laizer
Maktaba Ya Jamii Cheche

Mimi ninaitwa Emmanuel Laizer. Ndoto yangu inasema nitakapokuwa mkubwa nitakuwa mwalimu na rubani kwa ajili ya kuimarisha taifa halafu kuwasaidia wazazi wangu na kuwasaidia wanafunzi maisha ya baadaye kuwa mazuri.

1

Nataka kuwa mwalimu ili niwasaidie wanafunzi kufikia malengo yao ya baadaye. Pia nitaimarisha jamii na nchi na kulijenga taifa letu ili kupata fedha ya kusaidia jamii. Nataka jamii yangu iwe na furaha tele na jamii yangu isome kwa bidii.

2

Nataka kuwa na jamii ya wasomi. Halafu nataka kufika chuo.

Na nitakapokuwa mkubwa nitakuwa Mfaransa, Mmeru, na Mmaasai.

3

Nitakuwa na watoto 9. Halafu nataka kuwa na familia yenye furaha na amani nzuri. Familia yangu ipende kanisa na watoto wangu wasome kwa bidii.

4

Nataka kuishi Arusha kwa sababu ndoto yangu imeipenda na pia mwili wangu unapenda. Nataka kuishi Arusha kwa sababu nitakuwa karibu na wazazi wangu ili kuwasaidia kitu kilichowashinda na kuwatafutia chakula. Nitawasaidia wazazi wangu

5

kwa sababu nimefundishwa na wazazi wangu na wameniwezesha na kunilea hadi niwe hapa na kusaidia jamii. Nitasoma kwa bidii ili kunisaidia ndoto yangu ya baadaye na kusaidia jamii. Na natarajia kuwa na eneo la saiz yangu.

6

Nahitaji kuwa na lugha tatu ambazo ni Kifaransa, Kimeru, na Kimasai.

Nataka watoto wangu nao wasome kwa bidii na watoto wangu wasipende kununa. Nataka kusoma hadi chuo kikuu na familia yangu ipende kumwabudu mungu.

7

Naongea sasa kwa Kimaasai. Akaaji Emmanuel Laizer. Naakayu paaku olorew endeke oo mwalimuli le shule. Naakayu si paisoma mbaka pabaya chuo kikuu. Naakayu ore ingera ainei penyoru engai. Peeku eta engida tiatwa engai neeku eseryani.

8

Naakayu peeku familia i peningore elatya na butare. Akangidakino painguraki ingera ainei peraposho. Naakatengenwo teshule enikoni nichorai eramani.

9

Naakiretoki eramani nayetu ingwapi tofautitofauti.

(Kiswahili) Hadithi hii inahusu familia yangu isiwe na njaa na niwe nawatafutia chakula. Watoto wangu wasome na nitawasaidia. Familia yangu tuwe 9.

10
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Ndoto Zangu za Baadaye
Author - Emmanuel Laizer
Illustration - Maktaba Ya Jamii Cheche, Wanafunzi Wa Maktaba ya Jamii Cheche
Language - Kiswahili
Level - First paragraphs