

Ninaitwa Evalyne. Nilizaliwa 2015. Nilizaliwa Mtinko, mkoani Singida. Wilayani Mtinko, tunatumia Kinyaturu. Kwa mfano, Walatuni? Ntinala.
Baada ya kukua kidogo, bibi na mama walienda na mimi Moshi. Huko Moshi, tunatumia Kichaga. Kwa mfano, Shimboni shafo. Shisha.
Nilikuwa mtoto wa kwanza katika familia yangu. Nililelewa muda mfupi na mama yangu, kwa hiyo bibi yangu alinilea.
Mama yangu aliporudi, nilianza shule nikiwa na miaka 2 na nusu. Shule yangu iliitwa St. Karolass. Ilikuwa karibu na hospitali na Shule ya Msingi Msaada.
Baada ya miaka kadhaa, tulihamia wilaya ya Monduli ili nipate shule kwa sababu kulikuwa hamna shule ya Kiingereza.
Huko Monduli, tunatumia Kimaasai. Kwa mfano, Mama yeyo, takwenya? Iko.
Nilianza la kwanza nikiwa na miaka 6. Shule yangu inaitwa Meyer's. Shule ya Meyer's iko karibu na Shule ya Msingi Ngarash.
Wakati nikiwa darasa la kwanza katika Shule ya Meyer's, mwalimu wa darasa alikuwa akiitwa Wilifred.
Pia wakati nikiwa la kwanza niliisha na bibi yangu. Mpaka sasa ninaishi na bibi yangu.
Ninaipenda sana shule yangu na wazazi wangu. Sasa hivi nipo darasa la nne. Mwalimu wetu wa darasa ni Mwalimu Lalahe.
Mimi ninapenda masomo ya Kiingereza, Kiswahili, na sayansi. Mwalimu wetu wa shule ni Sista Chandrika Rose. Shule yetu hii ni ya masista.
Shule yetu tunatumia Kiingereza kwa wingi, na Kiswahili kidogo. Darasani kwetu tupo wanafunzi 54.
Nikiwa mkubwa ningependa kuwa mwalimu wa masomo ya Kiingereza na sayansi sana.
Mpaka sasa nina miaka tisa. Na nina mdogo wangu wa kiume. Jina lake anaitwa Alinanuswe. Mdogo wangu ana miaka miwili. Bibi yangu yeye anaitwa Lydia. Ana miaka 72.
Alikuwa mwalimu kipindi cha ujana wake.
Mama yangu yeye anaitwa Rose. Yeye ni mama mchungaji.
Na baba yangu yeye ni dereva.
Mimi nina mjomba wangu mmoja. Yeye ni mwalimu. Anafundisha Irkisongo.
Ninajua lugha mbalimbali, kama:
Kiingereza, mfano: How are you? I am fine.
Kinyaturu, mfano: Walatuni? Ntinala.
Kichaga, mfano: Shimboni shafo. Shisha.
Kiswahili, mfano: Za asubuhi? Salama/Nzuri.
Kimaasai, mfano: Mama yeyo, takwenya? Iko.

