Tunajua lugha nyingi!
Wanafunzi wa Maktaba ya Jamii Cheche
Wanafunzi Wa Maktaba ya Jamii Cheche

Unajua lugha zipi? Unazitumia wapi, ukiwa na nani, na kwa malengo gani? Unatarajia kutumia lugha zipi mbeleni?

Wanafunzi wa Maktaba ya Jamii Cheche walichunguza maswali haya kwa kina. Walichora ramani kuonesha matumizi ya lugha mbalimbali katika maisha yao, wakitumia rangi tofauti kuwakilisha lugha tofauti. Waliandika, kujadiliana, na kufundishana lugha zao. Matokeo ni kitabu hiki, pamoja na 'Lugha za Maisha Yetu,' vinavyoonesha uwezo wao mpana wa lugha mbalimbali.

1

Ninaitwa Evalyne. Ninajua lugha za Kinyaturu, Kiswahili, Kiingereza, na Kichaga.

At school, we are speaking English and Kiswahili. Na mwalimu anatufundisha Kiingereza na Kiswahili. Ninaongea na wenzangu kwa Kiingereza na Kiswahili kidogo.

At church, we are speaking Kiswahili. At home, we are speaking Kinyaturu, English, and Kiswahili. For example, what do you eat? Walatuni.

2

Lugha hizi zina umuhimu katika familia yangu kwa sababu zitanisaidia kufundishia na kuelewa lugha zangu vizuri. Nimejifunza sana lugha zangu kwa umakini mkubwa sana. Mfano chumvi kwa Kinyaturu inaitwa munyu. Salamu kwa Kichaga ni shimboni shafo, na unaitika shisha.

Mbeleni ninataka kujifunza lugha ya Kikorea, ili inisaidie kufanya kazi zangu.

3

Jamii haijui lugha yangu lakini nitawafundisha kwa sababu kila mtu ana lugha yake.

Kwenye picha hii, nimechora lugha mbalimbali, kama Kinyaturu: 'Lete munyu na maji' ni 'Leta chumvi na maji.' Na Ari ni sawa/haya/ndio. Kanisani tunatumia Kiswahili sana na Kiingereza kidogo. Nyumbani tunatumia Kiingereza, Kiswahili, Kinyaturu, na Kichaga. Ninapenda lugha zangu ninazotumia.

4

My name is Ayubu. Leo naongelea kuhusu lugha ninazojua. Ninajua lugha ya English, Kigogo, and Kiswahili. Kigogo natumia nikiwa Dodoma au nikiwa na mama yangu. Kwa sasa hivi nimesahau maneno mengine kwa sababu sijaenda Dodoma siku nyingi tangu nikiwa na miaka 7 mpaka sasa. Ninatarajia mwezi wa kumi na mbili mama akienda na mimi nitajifunza tena Kigogo. Lugha hii ina umuhimu kwangu kwa sababu ninaweza

5

nikaenda mahali pengine na nikawa sijui kitu wanachoongea kwa sababu sijui lugha wanayoongea. Na Kimaasai nimejifunza kwa rafiki zangu wakiwa wanachunga ng'ombe. Unakuta wanapeana zamu. Unakuta huyu akaenda kurudisha ng'ombe, ikafika zamu ya mwingine. Anamwambia kwa Kimaasai, "Nenda ukarudishe inkishu." Nikawa nawauliza, "Inkishu ndio nini?" Mmoja akaniambia, "Ni ng'ombe."

6

Na ninajua lugha ya English. Ninatumia nikiwa shuleni na mwalimu akiwa anafundisha darasani. Mbeleni ninataka kujua lugha za English, Kifaransa, Kichina, na Kijapani kwa sababu naweza nikakosa kazi ya jeshi nikapata rubani au kusafirisha mizigo kutoka China mpaka Tanzania. Sasa nikiwa naenda China na kupeleka bidhaa sasa nikawa sijui, nahitaji kujifunza ili niweze kupeleka bidhaa na kuchukua nilete Tanzania.

7

Ninategemea kutumia lugha ya English nikiwa nchini Uingereza, nikiwa ninafanya kazi zangu. Nitajifunza lugha hiyo nikiwa ninasoma vitabu vya kamusi ya Kiingereza. Ninajua maneno ya Kiingereza kwa mfano porridge ni uji. Ninategemea kujua lugha ya Kichina. Nikiwa daktari nikaitwa nikamtibu mtu halafu sijui kuongea lugha hiyo. Itabidi nijifunze na nitajifunza nikiwa nchini China.

8

Mimi ninaitwa Upendo. Ninajua lugha za Kimaasai, Kiswahili, Kichaga, na Kiingereza. Ndio ninatumia nikiwa nyumbani, nikiwa na bibi, nikiwa na marafiki zangu. Ni muhimu kujua lugha hizo. Nimejifunza nikiwa safarini, nyumbani, na shuleni. Maktaba inatufundisha kusema kichwa kwa Kichaga ni mro. Inatufundisha kusema kichwa kwa Kimaasai ni elukunya. Nitataka kujua lugha za Kimaasai, Kiswahili, na Kichina kwa sababu ninapenda kujua lugha kama hizo.

9

Ninataka kutumia lugha nikiwa safarini na nyumbani kwa sababu ninapenda kufanya kazi nikiwa naongea Kimaasai. Ninajua kusalimia kwa Kimaasai. Kusalimia kwa Kimaasai ni takwenya, iko, subai, iba. Nitafanya nikiwa ninapika chakula cha usiku au cha asubuhi na mchana au nikiwa ninakula chakula cha mchana au asubuhi na jioni. Ninajua lugha ya Kiingereza. Ninajua chungwa ni orange.

10

Mimi ninaitwa Kenton. Ninajua lugha za Kiingereza na Kimaasai. Shuleni ninatumia lugha za Kiingereza na Kiswahili. Nikiwa kwenye jamii ninatumia lugha ya Kiswahili. Nikiwa na mwalimu na marafiki zangu ninatumia lugha za Kiswahili na Kiingereza. Kimaasai ninatumia nikiwa na marafiki zangu.

11

Lugha hizi za Kimaasai na Kiingereza zina umuhimu mkubwa sana kwa sababu unaweza ukakwenda kwenye jamii ya Wamaasai na Wazungu na lugha hizi zinatusaidia.

Lugha ya Kimaasai nimejifunza kwa kuandikiwa na rafiki yangu tukiwa shuleni kwa sababu nilihitaji kujua lugha hiyo. Lugha ya Kiingereza nimejifunza kwa kufundishwa na mwalimu nikiwa darasani.

12

Kitu ninachoweza kukisema kwa lugha ya Kimaasai ni elukunya, enkaji. Kwa lugha ya Kiingereza nimejifunza kusema vitu mbalimbali, kwa mfano house, chair.

Mbeleni ninataka kujua Kichina, Kinyaturu, Kisukuma, na Kipare kwa sababu nazipenda lugha hizo. Ninatamani kutumia lugha hizo nikiwa nyumbani, kwenye jamii, na nikiwa ninafanya shughuli mbalimbali. Nitawaomba wanajamii wanifundishe.

13

Mimi ninaitwa Jesca. Ninafahamu lugha tatu ambazo ni Kiswahili, Kimaasai, na Kiingereza. Ninatumia nikiwa shuleni, kwa mfano Kiingereza na Kiswahili nikiwa nasoma, nikiwa na mwalimu pamoja na wanafunzi wengine. Lugha ya Kiingereza ina umuhimu wa kufahamu zaidi katika maisha yangu.

14

Lugha ya Kiingereza inanisaidia kufahamu vitu mbalimbali kwa Kiingereza. Nimejifunza lugha ya Kiswahili kwa kujadiliana na wanafunzi wenzangu na kwa kusoma vitabu mbalimbali. Kwa mfano star kwa Kiswahili ni nyota. Ninajifunza Kimaasai maktabani kwa kuimba nyimbo za Kimaasai.

15

Mbeleni natamani kufahamu lugha mbalimbali kwa mfano Kikenya na Kichina kwa sababu nataka kuishi nchi mbalimbali. Ninategemea kutumia lugha za Kichina na Kikenya nikiwa nyumbani nikiwa naimba. Nitajadiliana nikiwa na rafiki zangu ili kujifunza lugha hizo.

16

Ninaitwa Lionel. Ninataka kujua lugha za Kiswahili, Kimaasai, English, na Kichaga. Ninatumia lugha hizi nikiwepo shuleni na nyumbani, nikiwa ninafanya kazi mbalimbali, na nikiwa na walimu wa shuleni na maktabani. Lugha hizi nimejifunza maktabani na shuleni. Mimi ninataka kujua lugha ya Kichaga mbeleni kwa sababu itanisaidia maishani. Kwa kila lugha ninategemea nikiwa maktabani, shuleni, na nyumbani nitamfuata mwalimu Monica anielezee kuhusu lugha hizo.

17

Lugha ya Kimaasai ninajua kusalimia na kuongea na marafiki na ninatumia nyumbani. Kwa mfano, takwenya, iko, supai, epa. Na lugha ya Kiingereza ninajua kusalimia na kununua vitu. Kwa mfano mangoes maembe orange chungwa lemon limao food chakula pen peni pencil pensel house nyumba children watoto teachers walimu ball mpira exercise book daftari coach mwalimu wa michezo gas gesi. Ninajua Kichaga. Kwa mfano, mro kichwa makombe mabega.

18

Ninataka kujua Kikorea mbeleni kwa sababu kitanisaidia maisha nikiwepo ugenini. Kwa mfano, nikienda kusomea chuoni Korea. Nitaongea na walimu na wanafunzi. Na ninataka kuwafundisha ndugu zangu kuongea lugha ya Kikorea. Nikija kwenda nchi za mbali, kwa mfano China, ninataka kuongea Kichina pale ninapofanya jambo fulani. Kwa mfano, kujisomea, kuandika, kuongea na walimu na wanafunzi. Na pale sitakapoelewa nitamfuata mwalimu au mwanafunzi mwenzangu anieleweshe.

19

Mimi ninaitwa Safina. Kwa upande wangu mimi ninajua lugha ya Kiingereza. Najua maneno machache kwa Kiingereza kama vile kusalimia asubuhi na mchana. Ninatamani sana kusoma Kiingereza kwa mfano my name is Safina. Maana yake ni mimi ninaitwa Safina. Napenda kusoma vitabu vya Kiingereza. Ninatumia Kiingereza nikiwa shuleni na nikiwa nasoma darasani au nyumbani. Nikiwa na wanafunzi wenzangu wanapenda kusikia lugha ya Kiingereza wakati watu wengine wanasoma.

20

Lugha hii ina umuhimu wa kuongea na wageni kutoka nchi hizo wanazotokea. Nimejifunza lugha hiyo hapa hapa Monduli.

Napenda sana lugha yangu ya Kisukuma. Ninajua kusalimia kwa Kisukuma: mwadela mayo. Ni shikamoo mama kwa muda wa jioni.

Ninapenda kujua lugha za Kikorea, Kijapani, na Kiarabu, kwa sababu ya uwezekano wa kukutana na wageni kutoka nchi za nje. Napenda sana kusikiliza na mpaka nifikishe miaka 18 nitajua lugha hizo.

21

Ninategemea kutumia lugha hizo kama Kiingereza nikiwa Shinyanga nikiwa nawafundisha watu lugha nilizojifunza kama nilivyojifunza kwa kutumia wao. Nitajifunza kutoka kwa watu na wageni kutoka nchi tofautitofauti. Nikizitembelea nchi za Korea, Japan, na nchi za Uarabuni, nitafurahi sana kujua lugha hizo. Natamani kujua lugha hizo ili kuongea na watu kutoka nchi hizo na kutambua vitu vingi sana kutoka huko mbali na Tanzania.

22

My name is Pendo. Ninajua lugha za Kiswahili na Kiingereza. Ninajua pot ni chungu. Kimaasai nimefundishwa nyumbani na wazazi wangu. Lugha za Kiswahili na Kiingereza ninatumia nikiwa shuleni, nikiwa ninasoma na nikiwa ninauliza swali au kujibu swali.

Lugha hizi zote zina umuhimu kwa sababu unaweza kuelewa wakati wenzako wanakuongelesha lugha yoyote. Ninawafundisha gari kwa Kiingereza ni car, and people ni watu.

23

Ninajua love ni upendo. Tupende kujua lugha nyingi kwa sababu itatusaidia kuongea na wenzetu.

Mbeleni ninataka kujua lugha za Kimaasai na Kiingereza. Kwa Kimaasai ninajua moja hadi nne. Ninajua nabo, are, uni, ongwani. Ninataka kujua lugha za Kifaransa na Kigogo ili niweze kuongea. Ninawaomba watu wanaojua wanifundishe lugha hizo kwa sababu inanisaidia kwenye maisha yangu. Ninapenda kusoma sana vitabu vya hadithi.

24

Ninajua kusalimia kwa Kimaasai. Ni takwenya na marahaba kwa Kimaasai ni ikool. Kimaasai ndio lugha yangu. Nimefundishwa na shangazi, mjomba, babu, bibi, mama mdogo, mama, na baba. Naipenda sana lugha yangu kwa sababu itanisaidia sana.

Pia ninajua lugha ya Kiingereza ili nikamilishe kipaimara. Ninafurahi sana kuongea lugha nyingi mbalimbali. Asante sana kwa kunisikiliza. Thank you very much!

25
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Tunajua lugha nyingi!
Author - Wanafunzi wa Maktaba ya Jamii Cheche
Illustration - Wanafunzi Wa Maktaba ya Jamii Cheche
Language - Kiswahili
Level - Longer paragraphs