Hapo zamani za kale walitokea marafiki wawili ambao ni Sungura na Fisi.
Siku moja marafiki hao walienda kutafuta chakula, Kwa bahati mbaya walikosa.
Sungura na ujanja wake alimshauri Mzee Fisi kwamba wakawale mama zao.
Fisi kwa tamaa na upumbavu wake alienda kweli na kumchinja mamake na kumla.
Sungura yeye hakufanya hivyo Bali alienda kumficha mama yake.
Baada ya Fisi kumchinja na kumla mamake alirudi kwa Sungura na kumwambia kuwa tayari amemla mama yake.
Sungura alimcheka Sana,ndio maana mpaka leo Sungura na Fisi ni maadui.