Esta na Jitu ndotoni
ONOROTA INNOCENT
ONOROTA INNOCENT

Paukwa pakawa, Esta alikua ndotoni "ewe Shila nakuita" Shila aliitika kwa sauti kuu, ghafla jitu kubwa lilitokea.

1

Mdomo wake ulikua mithili ya panga, urefu wake ulipita magorofa marefu, hakika aliogopesha.

2

Esta alishuhudia jitu hilo likimeza fuso na kutafuna pamoja na vioo vyake, kila mmoja alikimbia huku na kule yalikua machafuko makubwa.

3

Jitu hilo halikuridhika, lilibeba watu sita na kuwatafuna mithili ya kumbikumbi wachache kinywani. Kila mtu alipigwa na butwaa.

4

Ghafla esta alikurupuka kutoka usingizini.

5

Esta alikurupuka kutoka usingizini alipigwa kelele kuu.

6

Mama yake alikurupuka kutoka usingizini.

7

Esta alimuhadhitia mama yake kuhusu ndoto yake.

8

Mama yake akasema ulifikirialo linyamazia, likitokea lihadithie.

9

Esta alibembelezwa na mama yake na kurudi kitandani mwake kulala.

10

Esta alilala usingizi mnono mpaka asubuhi.

11
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Esta na Jitu ndotoni
Author - ONOROTA INNOCENT
Illustration - ONOROTA INNOCENT
Language - Kiswahili
Level - First paragraphs