

Mimi ni Kelvin Yona, Monduli yetu ni miti mingi, watu wengi na halo mzuri ya hewa.
Mimi ni Nengaripo Memusi Karani,Monduli yetu ni bustani zinazopendeza sana pamoja na nyumba nzuri.
Mimi ni Merry Beatus Make, Monduli yetu ni mimea kwa sababu inaweza kutuletea mvua nyingi, na kutuondolea ukame, pia mimea inafaida nyingi mfano;(1) kutupatia mbao, (2) kutupatia kuni, (3) kutupatia hewa safi.
Mimi ni Nakaji Memusi, Monduli yetu ni majengo kwasababu kuna majengo yenye thamani, na pia kuna misitu mizuri inayopendeza na yenye wanyama.
Mimi ni Leonard Paulo Rafael, Monduli yetu Ina viwanja vya mipira kwa mfano sabasaba,lashaine, ngarash,Chuo cha CDTI na kadhalika.
Mimi ni Noel Wesesilaus Mtaki,Monduli yetu ina majengo.
Mimi ni Josephu Jonathan, Monduli yetu ni milima na miti.
Mimi ni Wentworth Maurice Mwita, Monduli yetu ni mafundi na maji.
Mimi ni Jofrey Hamisi, Monduli yetu ni shule nzuri za sekondari zakuvutia.
Mimi ni Jenifer Daniel Mollel, Monduli yetu ni stadi za maisha na ubunifu wa vitu
Mimi ni Marvin Loth, Monduli yetu ni shule nzuri za msingi za kuvutia
Mimi ni Magdalena Pusindawa Mollel, Monduli yetu ni mazingira na madhari nzuri ya kuvutia yenye hewa safi.
Mimi ni Mseyeki Misila Mollel, Monduli yetu ni familia zenye mshikamano na upendo kila siku.
Mimi ni Salome William Mollel, Monduli yetu ni familia na ufugaji unaopendeza

