Harusi iliyofana
Judy
Judy

Ilikuwa siku ya Jumamosi. Nilienda na rafiki zangu
kuhudhuria harusi ya jirani yetu, Nekesa.

Tulipofika huko, tuliona wazee wakijiburudisha kwa kahawa chungu.

"Aha! Kweli siku njema huonekana asubuhi," tuliwaza.

1

Tuliyoyaona yalikuwa yakufurahisha. Mwamamke mmoja alimwita rafiki yangu aliyekuwa karibu naye.

Alimwuliza ikiwa tulikuwa tumekunywa chai tayari. Mwanamke huyo alipogundua kuwa hatukuwa tumekunywa chai, alisema, "Nenda haraka ukawaite hao wenzako."

2

Baada yakunywa chai tulipanda garini kwenda kanisani kwa ajili ya kushuhudia ndoa hiyo.

Hapo kanisani kulikuwa na mlolongo wa magari na halaiki kubwa ya watu.

Ibada ilipoanza ilikuwa saa tatu asubuhi.

3

Kasisi alikuwa amefika kanisani kwa ajili ya sherehe hiyo. Nekesa na mchumba wake Steve walikuwa wanang'aa kama mbala mwezi.

Steve aliahidi kuwa hangemfanya kuwa ngoma. Wakati tulioungojea uliwadia ulikuwa wakati wa kukata keki.

4

Nekesa alikata keki pamoja na mumewe. Tulikula keki pale kanisani na tukaanza safari ya kwenda nyumbani.

Tulipofika huko tulicheza mziki kwa furaha. Tuliwatakia maharusi maisha mema.

5

Nilikuwa na njaa sana, tulikula kila mtu shibe yake. Pia tulikunywa kinywaji kilichokuwa kitamu sana.

Baada ya hayo yote, tulirudi nyumbani tukiwa na furaha chungu nzima.

6
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Harusi iliyofana
Author - Judy, faith ziro Elvinah, Jasmine kuvuna
Illustration - Judy, faith ziro Elvinah, Jasmine kuvuna
Language - Kiswahili
Level - Longer paragraphs