

Hapo zamani za kale paka na mbwa waliishi pamoja katika nyumba ndogo. Wanyama hawa walikuwa na zamu ya kupika na kuchota Maji mtoni.Wanyama hawa walikuwa wakulima walimeesha mimea mbali mbali kama vile mahindi maharagwe,pojo na viazitamu.
Siku moja mbwa alikua katika zamu yake ya kupika chakula naye paka akawa katika zamu yake ya kwenda kuchota maji mtoni. Paka aliondoka na kwenda mtoni kuchota maji.
Paka aliporudi kutoka mtoni alimkuta mbwa akiwa akimsubiri.Paka aliepua ndoo na akaketi kumsubiri mbwa ampakulie chakula.
Mbwa alipomuona paka akisubiri chakula,alitimua mbio kwa sababu alikua amepika chakula Kisha akakila chote.Paka alimshangaa mbwa paka alienda mahali walipokua wakipikia chakula.Alifungua chungu walichokua wakipikia hakukua na chakula.
Paka alimwendea mbwa mbio lakini hakumuona,alikua amekimbia.Kuanzia siku hio hadi Leo paka akimwona mbwa anampiga alipize kisasi.

