

Hapo zamani za kale,aliishi mtu mmoja Jina lake Karisa.Mtu huyu alikuwa tajiri sana.Alikuwa na mashamba mengi ,mifugo na majumba ya kukodi.Karisa alikuwa tajiri Ila alikosa vitu fulani kwenye maisha yake.
Hakuwa na mtoto kwa sababu eti alikuwa gumba ila ni kwamba hakutaka kuoa.Watu wa Kijiji alichoishi walimwambia kuwa aoe ili apate mrithi wa mali zake.
Karisa aliposikia hayo aliwatukana watu hao akisema, "Nilipokuwa nikitafuta huu utajiri huyo mrithi alinisaidia?",Nilitafuta mwenyewe Kwa hivyo niacheni niponde Mali yangu mwenyewe.
Mara nyengine mtu angejaribu kumwambia angemtukana na kumtishia kwamba akisikia anaongea upuzi huo tena angemshitaki.Watu waliamua wamwache Karisa na maisha yake. Karisa hakuwa mkarimu.
Hakutaka kuwasaidia watu waliohitaji msada kutoka kwake.Karisa aliendelea kuponda Mali yake kama kawaida . Alizitumia pesa zake Kwa wanawake na kwenye mabaa.Siku zilisonga ,miezi ikaenda Na miaka ikapita.
Karisa alikuwa anaanza kuwa mzee sana .Alipoona hivyo akamua afanye kitu.Alikaa akawaza na kwakua mwishowe akapata jawabu .Aliamua auze Mali yake yote.Alitafuta mteja ambaye angemuuzia mali yake
Baada ya siku tatu alimpata huyo mteja.Alimuuzia mali zote Kwa laki hamsini.Karisa alipopata pesa hizo aliamua kwenda nchi ya mbali.Huko aliishi kwenye nyumba ya kukodi.Alilazimika kulipa elfu hamsini kila mwezi.
Pia angenunua chakula na vitu vyengine alivyohitaji kutumia pesa hiyo.Baada ya miezi michache pesa ilimwishia.Hivyo basi hakulipa pesa ya nyumba.Hatimaye alifukuzwa kwenye nyumba hiyo.Hapo mzee Karisa alikosa mahali pa kuishi na chakula .
Alilala nje kila siku Na kulipokucha alizunguka na kuomba chakula.Mara nyengine alilala njaa afya yake ilidorora alikonda kama Ng'onda Kwa kuwa hakuwa amezoea maisha hayo ya umaskini.Watu walipomwona hawakumsaidia na chochote.
Wengi walimcheka Kwa sababu ya alivyokuwa.Kwa kuwa mzee Karisa hakuwasaidia watu, hao pia hawakumsaidia.Mzee Karisa alilipwa kulingana na matendo yake.
Mzee Karisa aliugua ugonjwa uliosababishwa na baridi iliyompiga usiku na njaa aliyokuwa nayo.Alijuta kwanini hakusikiliza ushauri aliokuwa akipewa.Aliugua mpaka akaaga Dunia.Hapo ndipo ilipobainika kuwa tamaa mbele mauti nyuma

