Harusi ya kuvutia
Murimi Kimanthi
Brian Wambi

Tuliamka mapema kabla ya jogoo wa kwanza kuwika. Tulikuwa na hamu kubwa sana kwa sababu ilikuwa siku ya harusi ya dada yangu.

Dada yangu alikuwa anafunga ndoa na kijana mtanashati. Kijana huyo alikuwa mwenye heshima.

1

Tulienda kujiandaa kwa uharaka kwa sababu tulijawa na furaha. Baada ya kujiandaa, tulijitazama kwenye kioo. Kisha tukavaa nguo za kupendeza.

Tulionekana wa rembo sana. Baadaye tulielekea kwenye harusi katika gari la kipekee.

2

Kulikuwa na umati mkubwa wa watu. Kulikuwa kumepambwa kwa kutumia baluni na mapambo mengineyo mengi.

Bwana harusi alikuwa amevalia suti ya bluu, shati la manjano na tai ya madoadoa. Alikuwa ameng'ara.

Muda sio mrefu, wakati ambao watu walisubiri kwa hamu, ulifika.

3

Bibi harusi aliwasili akiandamana na wapambe wa kikike. Wote walikuwa wamevalia hereni masikioni na kupaka poda usoni na rangi nyekundu midomoni.

Ungewaona, ungedhani walikuwa wamelamba damu. Walikuwa warembo sana. Bibi harusi alivalia veli nyeupe pepepe.

4

Machoni alipaka wanja, kwenye viganja alivalia gilavu nyeupe pepepe. Lakini, athari za hina zilionekana mikononi.

Nyweleni alifunga chupio maridadi sana. Kwa umbali niliona alikuwa kupaka ngeu nyweleni.

5

Mziki ulichezwa na wapambe wale walitangulia kuingia ukumbuni. Walifuatwa na Bibi harusi aliyetembea polepole akaingia ukumbuni.

Alipofika kwenye madhabahu, wazazi wetu walimwelekeza.

6

Walipiga magotii na wakaanza kuomba. Baadaye waliunganishwa na kasisi na kuwa mme na mke.

Baada ya kuvishana pete, walienda kutia sahihi cheti cha ndoa.

Hatimaye, wakatoka wakiwa wanaimba na kucheza ngoma za furaha.

7

Tulianza safari ya kwenda hotelini. Tulipofika hotelini tuliwaona Bibi harusi na Bwana wakipakuliwa chakula.

Tulikula na kucheza ngoma zaidi. Baadaye tulianza safari ya kwenda nyumbani kwa maharusi.

8
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Harusi ya kuvutia
Author - Murimi Kimanthi, Warren Ochieng, Joab Ziro
Illustration - Brian Wambi, Leo Daly, Magriet Brink, Salim Kasamba
Language - Kiswahili
Level - Longer paragraphs