

Hapo Zamani zakale kulishi mzee mmoja aliyeitwa matao .Kijiji Chao kilitwa matukio.Mzee matao alikuwa mjasiri kwakua hakuogopa kitu chochote.
Katika Kijiji cha matukio kulikuwa Na nyoka mkubwa sana
Aliye meza mifugo ya wanakijiji .
Nyoka huyo aliitwa chatu .Chatu Ni mnyama hatari sana.
Mnyama huyo aliishi kwenye pango kubwa kwenye shamba la matao.Siku moja,matao alikuwa njiani
Akirudi nyumbani alikuwa ametoka shambani .Alimwona
chatu huyo na akaamua kumpangia siku ya kumwua .siku hiyo
Ilikua ya kwanza kumwona .Siku ya Kwanza ikapita ,siku ya pili ikapita,siku ya tatu ndipo aliamka alfajiri na mapema akabeba .
Panga,fimbo Na mshale Na akaanza safari .
Alipofika, alifika sawa sawa na chatu huyo alikuwa akitoka.Mzee matao alitoa fimbo yake alimfuata nyoka hadi akampata alimpiga fimbo tatu chatu yule akafariki palepale alipo maliza kumwua chatu.
Alienda kuwatarifu wanakijiji walifurahi kusikia hivyo.Kijiji cha matukio kilirudi kama mwanzo waliishi Kwa amani wanakijiji waliamua kumtolea sherehe kubwa mzee matao mzee matao alifurahi sana akawambia wanaume wote wa Kijiji cha matukio
Waoga,wawe jasiri wa kila kitu.

