

Bi Komwe, Bwana Juma, Bi Sidi na Bwana Kolombo waliishi katika kijiji cha Mwezangombe. Walikuwa wameharibu mazingira kwa muda mrefu.
Kila siku walielekea msituni na kukata miti.
Siku moja walielekea msituni asubuhi. Siku hiyo chifu alisikia habari hizo akawajulisha afisa wa polisi.
Polisi waliwakamata wanne hao na kuwapeleka katika kituo cha polisi.
Baada ya hapo walielekea mahakamani. Chifu aliwaita watu wote wa kijijini. Umati mkubwa ukakusanyika.
Chifu alielezea kuhusu miti akisema kwamba miti ni muhimu kwa viumbe vyote.
Alielezea jinsi miti hutusaidia kwa mambo mengi kama vile hewa safi, kuleta mvua, matunda, dawa, kuni, makaa, kivuli na mbao.
Siku hiyo sote tulijifunza mengi kuhusu miti. Bwana Chifu alionya, "Atakayepatikana akikata miti, atapewa adhabu kali na kwenda gerezani."
Hilo lilikuwa onyo kali kwa kila mwanakijiji.
Kila mtu alimshukuru Bwana Chifu na kuondoka.
Watu wale walifungwa gerezani miaka mitano kwa kukata miti.

