MTO TORIA
Fatma Maleta
Salim Kasamba

Hapo zamani za kale , katika mji mmoja kulikuwa na mto wa maajabu sana,maji yake yalikuwa tiba ya magonjwa mengi.
Mto huo ulitiririka vizuri mpaka ulipoingiliwa na makazi ya watu. Mzee Pilo alianza ujenzi kando kando ya mto na kuishi hapo.

1

Mto huo ulikuwa unaitwa mto Toria na ulijawa maajabu mengi mno .Katika Mto huo waliishi viumbe tofauti Kwa Upendo mkubwa sana.

2

Basi watu walivyoona Kuna watu waliishi pale na kunufaika na mto huo Kwa kupata chakula, makazi , na hewa safi wakaamua na wao wajenge kando kando ya mto huo .Wakazi wengi wakaanza kufanya hivyo

3

Kutokana na uharibifu wa mazingira, mafuriko makali yakatokea na kuhatarisha maisha ya viumbe wengi na kufanya mto ule kusababisha madhara zaidi

4

Uharibifu wa mazingira ukafanya mto uliojawa na uhai kukauka na viumbe wengi kupoteza maisha.
Njaa, ukame , uharibifu wa mazingira, mafuriko na madhara mengi yakatokea kutokana na kutotunza mazingira yetu na maafa mengi zaidi yakafuata.

5

Maswali

1.Je wewe unadhani kwanini tutunze mazingira?



2.Kuna faida gani za kuishi mazingira
safi?



3.Je tufanye nini kulinda mazingira yetu?




4.Nini umejifunza kutokana na kitabu hiki?

6
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
MTO TORIA
Author - Fatma Maleta
Illustration - Salim Kasamba, Rob Owen
Language - Kiswahili
Level - First paragraphs