Kisa cha Sungura na Fisi
Marvin Edward
Marvin Edward

Hapo zamani za kale, palikuwa na marafiki wawili: Sungura na Fisi. Walikuwa wanapendana sana.

1

Siku moja, Fisi alimwambia rafiki yake Sungura, "Twende shambani tukalime."
Sungura akakubali waende.

2

Sungura akamwambia, "Twende tukapike chakula kwanza, ndio twende shambani." Fisi akakubali wakapike.

3

Walivyomaliza kupika wakaenda shambani.

4

Walivyomaliza kulima, Sungura akasingizia tumbo linamuuma.

5

Fisi akamwambia Sungura aende nyumbani, lakini Sungura hakuenda nyumbani. Alienda kula chakula kidogo. Sungura akarudi shambani. Fisi akamwuliza, "Rafiki yangu, tumbo limepona?" Sungura akasema, "Ndiyo." Wakaendelea kulima.

6

Sungura akasingizia tena tumbo linamuuma. Fisi akasema, "Nenda ukalale." Sungura akaenda kula chakula chote, halafu akaenda kulala.
Fisi akamaliza kulima, halafu akaenda kula chakula. Alivyoenda hakukuta chakula. Kilikuwa kimeliwa chote.

7

Fisi akaenda kumwuliza Sungura, "Wewe ndio umekula chakula?" Sungura akajibu, "Hapana." Fisi akanyamaza.

8

Fisi akaenda kupika chakula. Chakula kilipoiva, Fisi akamwambia Sungura, "Rafiki yangu, njoo tule chakula." Sungura akasema, "Nimeshiba." Fisi akamuliza, "Umekula nini?" Sungura akasema, "Nimepika chakula." Fisi akala chakula chote.

9

Wakaenda kulala. Usiku ulivyofika, Sungura akaanza kuharisha. Fisi akasema, "Umekula nini?" "Sijala." Fisi akamwambia, "Huwezi kuharisha bila kula kitu. Wewe ndiye umekula chakula tulichopika ndio maana tumbo linakuuma."

10

Fisi akamwambia, "Ondoka hapa. Wewe siye rafiki yangu."

Tangu siku hiyo, Sungura na Fisi ni maadui. Fisi akimuona Sungura anamkimbiza.

11

Naitwa Marvin Loth. Nina miaka 12. Ni mzaliwa wa Monduli, mkoani Arusha. Ninasoma darasa la 6 Shule ya Msingi Sinoni.

Vipaji vyangu ni kuchora na kucheza mpira wa miguu. Nilitunga hadithi hii baada ya kusoma vitabu vingi Maktaba ya Cheche.

12
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Kisa cha Sungura na Fisi
Author - Marvin Edward
Illustration - Marvin Edward, Benson Laizery
Language - Kiswahili
Level - Longer paragraphs