

Hapo zamani za kale palitokea vijana wawili, waitwao Samsoni na Samweli.
Walikuwa wakisoma Shule ya Msingi Songambele. Vijana hawa walikuwa wakisoma darasa la sita. Shule yao ilikuwa ni shule ya bweni.
Walikuwa hawapendani.
Walipewa hela ya matumizi shuleni. Samweli alikuwa akiiba hela ya Samsoni.
Siku moja, Samsoni alitaka kumtega Samweli anapomwibia. Akaweka pesa yake ndani ya box la kalamu.
Samweli alipoingia kwenye chumba chao cha kulala, akakuta sanduku la Samsoni. Akafungua na kupangua vitu vya Samsoni. Akainua lile box na akaona pesa ndani ya lile box.
Kumbe Samsoni alikuwa dirishani akimwangalia.
Samsoni akaingia na kumwambia, "Siku za mwizi ni arobaini." Samweli akamwambia, "Nisamehe. Ni mimi niliyekuwa nikiiba hela zako. Nisamehe sana. Sitarudia tena kukuibia ndugu yangu."
Kuanzia siku hiyo walipendana na kuheshimiana.
Hata shule ilipofungwa walirudi nyumbani pamoja.
Ninaitwa Benson. Ni mzaliwa wa Monduli, mkoani Arusha. Nimemaliza la 7 Shule ya Msingi Ngarash.
Nia ya kuandika hadithi hii ilitokana na kusoma vitabu vingi Maktaba ya Cheche. Utungaji wa hadithi ni njia ya kukuza Kiswahili, lugha ya taifa.

