Marafiki Wawili: Sungura na Fisi
Kelvin Yona
Kelvin Yona

Hapo zamani walitokea marafiki wawili ambao ni Fisi na Sungura. Walikua ni marafiki wazuri sana.

1

Walikua wanakwenda kutafuta chakula pamoja.

2

Siku moja, Fisi aliumwa sana. Hakuweza kula wala kunywa. Sungura alimhimiza sana ale, kwa maana asipokula atakufa.

3

Siku tano baadaye, Sungura alizaa watoto watano. Fisi alitamani kuwala watoto wa Sungura.

4

Siku moja, Fisi alipona lakini alijifanya anaumwa. Sungura alikwenda kutafuta chakula kwa ajili ya watoto wake pamoja na Fisi.

5

Aliporudi aliwakuta watoto wake watano hawapo. Alimwuliza Fisi, "Watoto wangu wako wapi?" Fisi alijibu, "Sijui. Itakuwa wameenda kucheza." Kumbe Sungura alishajua kuwa Fisi amewala wote.

6

Kuanzia hapo Fisi na Sungura walikua maadui.

7

Ninaitwa Kelvin. Nimezaliwa Monduli, Arusha. Ninasoma darasa la nne Shule ya Ngarash. Nina miaka 11.
Nimeandika kitabu hiki Maktaba ya Cheche. Ninapendekeza watoto wajitahidi kutunga hadithi ili kuwasilisha mawazo yao na kupanua Kiswahili.

8
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Marafiki Wawili: Sungura na Fisi
Author - Kelvin Yona
Illustration - Kelvin Yona
Language - Kiswahili
Level - First paragraphs