Mto wa ajabu
Hillsville Darasa la saba
Hillsville Darasa la saba

Hapo zama za babu, palikuwa na msitu. Katika msitu huo palikuwa na mto wa kipekee. Mto huu ulikuwa wa ajabu. Wanyama walioishi kwenye huo msitu walipenda kuutazama lakini ilikuwa vingumu kufika karibu kwa kuwa ulikuwa na malkia.

1

Miaka nenda miaka rudi, wanyama walijaribu kufikia msitu huo ingawa juhudi zao hazikufua dafu. Haja yao ilikuwa kuvuka ile ng'ambo ingine kwa kuwa upande wao ulikuwa mkavu.

2

Walitamani Kula majani mabichi na kulala chini ya kivuli.

3

Siku moja malkia aliyekuwa anaishi mtoni kwenye msitu huo alifikiria kwenda kuwasadia wanyama ambao waliokuwa pande iliyokuwa kavu. Alipanga safari yake kwa muda wa siku mbili.

4

Ala! Alishangazwa sana na mambo aliyoyaona. Alipata wanyama wengi wakifa kwa janga. Dunia yao ilikuwa kavu. Alijawa na hasira papo hapo akageuza rangi yake kuwa ya kijani.

5

Malkia huyo alitandaa kote, na kila alipopita paligeuka kuwa kama pande hiyo nyingine ya mto. Nyasi ilimea na miti iliyokauka kurudisha uhai na kujawa na majani mabichi.

6

Wakati alipokamilisha kazi yake iliyomtuma pande hiyo alirudisha rangi yake ya kawaida iliyokuwa hapo awali. Alifurahia sana Na kung'aa kama nyota kuelekea mtoni.

7

Siku moja Wanyama walienda kwenye mto kunywa maji. Malkia alitokelezea kwa ghafla na kuwaambia wanywe maji na pia wao watang'aa kama majani mabichi.

8

Malkia alifurahia sana kujulikana na wanyama na kuwa hawakumuogopa tena. Waliishi maisha mema ya amani msituni.

9

Alipofika mtoni pahali alipokuwa akiishi alipata makao yake yametayarishwa na akaingia ndani ya maji na kuungana nayo kisha yakawa matulivu.

10
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Mto wa ajabu
Author - Hillsville Darasa la saba
Illustration - Hillsville Darasa la saba
Language - Kiswahili
Level - First paragraphs