

Hapo zamani za kale kuliishi mzee mmoja aliyeitwa mzee TAMAA. Mzee huyo alikua na tamaa na ulafi kupimdikia. Alienda kwa kila sherehe na anakula kila kitu na asishibe. Alikua anakunywa kila kitu na asishibe sababu ya tumbo lake kubwa ajabu.
Mara nyingi akiwa kwake alikua anaketi huku akiwaza na kuwazua kuwa atakula wapia? Akikumbuka kuwa kuna sherehe kijiji jirani anaoga na kuenda kwa iyo sherehe kukula na kukunywa. Mzee TAMAA alikua na tamaa kama ya fisi na ulafi kupindukia.
Alipokua barabarani alikutana na mtoto mmoja akamwelezea kuwa kuna sherehe kijiji mwao. Mzee Tamaa akashindwa aende wapi asiende wapi. Aliwaza na kuwazua huku mate yakimdodoka kama fisi. Mzee tamaa akaamua kuenda kijiji jirani kwanza kukula
Alipofika kwa sherehe kijiji jirani akapata bado chakula kupakuliwa. Alipata bado mchele ama chai kuiva. Akarudi mbio huku anaomba moyoni mwake asipate kama chakula kimeisha. Aliharakisha na kukimbia mbio angalau akule sherehe zote hizo.
Mzee tamaa alipofika kwa sherehe ya pili alipata kuwa wamekwisha kula na kuosha vyombo. Akaketi chini huku jasho likimtoka. Aliwaza na kuwazua kisha akaamua kuenda kwa sherehe ya kwanza kukula huko. Alitoka mbio tena na kurudi kwa sherehe.
Mzee tamaa alikimbia sana na kuchoka. Akiwa ameshtuka sana huku akidondoka na jasho jingi mwilini mwake. Aliomba sana chakula kisiwe kimeisha kwa sababu masaa yalikua yamesonga kweli kweli na pia njaa ilimwandama sana. Mzee tamaa alifika.
Mzee tamaa hakuamini alichokiona. Sherehe ilikua imeisha na vyombo vikaoshwa tayari kurudishwa makwao. Aliwaomba mabaki lakini mbwa walikua washakula kila kitu. Aliomba chai akapata pia imekwisha kitambo. Mzee tamaa akaamua kurudi kijijini.
Mzee tamaa alitembea pole pole kwa kuwa alikua amechoka sana. Kufika kwa kijiji mwake akapata watu walirudi nyumbani kwao na sherehe iliisha kitambo. Aliketi na kulia sana sababu alikosa chakula kwa sherehe zote mbili. Akaamka akaenda kwake

