

Hapo zamani za kale paliishi nyanya na kijana mmoja.Waliishi katika kijiji cha Bora. Kijana huyo alikuwa mtiifu sana shuleni na hata nyumbani. Yule kijana alimpenda nyanya yake sana,angemfanyia nyanya yake chochote akitakacho.
Yule nyanya alikuwa na ugonjwa wa rabua. Nyanya alikuwa anaamtuma yule kijana ampe maji anapoitaji, na kila wakati nyanya akiitaji dawa yule kijana anamtengenezea. Nyanyake akaamua kumtuma kwa msitu wa mugambo uliombele ya mto mkubwa.
Nyanya yake alimwambia maneno matatu atakayo fuatilia akiwa safarini.la kwanza; hukiona pangoni husilale huko,la pili hukiona shinda chukua hii kjiti nitakayo kupa hurushe juu na hutasaidika na la tatu akampa kifagio akiona maji hutambeba.
Kijana alimuaga nyanyake. Nakufunga safari yake kuelekea msituni. Kijana alipofika kwa mto alichukua kifagio na kukalia akavukishwa maji. Aliendelea na safari hadi akafika kwa mti wa matunda alikuwa amehisi njaa na alikula matunda yale.
Kijana alipofika kwa ule mti alikuwa ameambiliwa, alipanda ule mti na kuchuna tawi moja kubwa na kushuka. Yule kijana alifunga safari yake kurudi nyumbani kwa nyanya yake. Safari yake ilimchukua hivi masaa kumi na mawili kurudi nyumbani.
Baada ya safari yake refu, yule kijana alirudi nyumbani na kumpata nyanya yake salama akiwa ametulia kwa kitanda. Kijana akampa nyanya yake lile tawi. Nyanyake alimwambia amutengeneze dawa kutoka kwa lile tawi na kijana akalitengeneza dawa.
Kijana alipotengeneza dawa alimpa nyanya yake, akapona nakumbariki kijana. Kijana aliendelea kuishi na nyanya yake.Siku moja kijana aliambia nyanya anaenda kutafuta kazi nyanya akambariki afahuru maishani kisha akamuaga nyanya yake.

