MAISHA BAADA YA MATESO
Jennifer Kendi
Jennifer Kendi

Hapo zamani paliisha mzee aliyeitwa Joni. Aliishi kitongoji mwa kijiji cha Maweni. Alikua na mke ambaye hakua na mtoto. Joni aliomba mungu sana awabariki na mtoto angalau mmoja. Baada ya miaka miwili Joni walibarikiwa na mtoto Bahati.

1

Baada ya miaka mitano Bahati alianza kuenda shule. Alisomea shule inaitwa Tusome ambapo alikua akiongoza kwa masomo na michezo. Alikua mtiifu na mwenye adabu sana na kila alipokutana na mtu mzee alimsalimia kwa heshima na adabu ya juu sana.

2

Bahati alipofika darasa la nane mamake alipatwa na maradhi na kuaga dunia. Joni na bahati walipatwa na uzuni sana.Baada ya mazishi Joni alioa bibi mwingine aliyekua na msichana mmoja aliyeitwa Asha. Asha alikua mvivu sana na roho chafu.

3

Alichokifanya ni kutoka nje na na kuota jua kisha anamwambia Bahati amletee chai na kumtesa. Siku moja Bahati akiosha vyombo mamake wa kambo alikuja na kumwaga hizo vyombo chini. Maskini Bahati alipata taabu sana na kuteseka kweli kweli.

4

Siku moja Bahati alitoka shuleni na kumkuta babake amelala. Akamuuliza babake yake shida iko wapi?Akajibu yeye ni mgonjwa.Bahati akaita mamake wa kambo ambaye alimchukua akampeleka hadi hospitalini.

5

Walipofika hospitalini mzee Joni alipimwa na akaonekana na ugonjwa wa kisukari. Daktari alianza kumpa matibabu papo hapo. Bahati alimwagalia kwa huzuni huku akilia kwa huruma na kumwombea. Baada ya wiki mbili walirudi nyumbani akapumzike

6

Daktari alimwelezea Mamake Aisha kuwa mzee Jona alishwe vyakula vyenye nguvu. Baada ya mwezi mmoja mzee Joni alipata nafuu. Siku moja Mamake Aisha alimfukuza Bahati kwenda kutafuta kazi.Bahati alilia sana huku akidondoka na machozi usoni.

7

Bahati alipokua barabarani alikutana na mtoto wa mfalme. Alimwulizia kuwa anaenda wapi akilia. Bahati akamwelezea kila kitu. Kisha mtoto wa mfalme akamwomba hawe mke wake. Bahati aliolewa na mtoto wa mfalme na akaishi maisha ya starehe sana

8
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
MAISHA BAADA YA MATESO
Author - Jennifer Kendi
Illustration - Jennifer Kendi, Goodluck Kirimi, Traccy Kairuthi
Language - Kiswahili
Level - First paragraphs