KIJANA MTIIFU
Traccy Kairuthi
Traccy Kairuthi

Hapo zamani kulikua na Kijiji kimoja. Kijiji hicho kuliishi wakulima na madaktari. Kando ya hicho kijiji kulikua na jumba moja ya dhahabu. Kwa hicho kijiji kulikua na kijana mmoja aliyeitwa Ali ambaye aliishi na shangaziye kwa hicho kijiji

1

Siku moja Ali akitembea kutafuta kazi alishtuka sana kuona jumba kubwa la dhahabu. alifika pale na kubisha mlango akiuliza nani ako ndani. Msichana alitokea na Ali akamuulizia anaitwa nani. Alijibu anaitwa zuhuri na tabasamu lisilokauka

2

Mfalme alipomuona Ali alishtuka sana na kumwuliza kuwa anataka nini. Alijibu kuwa anatafta kazi ili wapate chakula. Mfalme alimwambia kuwa arudi siku ingine na atampa kazi ya kufua nguo. alirudi keshowe kuomba kazi kwa uyo mfalme

3

Alipata kazi ya kufua nguo na kila alipomalizia kufua alilipwa pesa na dhahabu, alijengea shangaziye jumba kubwa na akamshukuru mfalme kwa jambo hilo sana. Ali aliwasaidia wanakijiji kwa kuwajengea na pia kulipia watoto wao karo ya shule

4

Wakulima waliendelea na kazi yao ya ukulima huku madaktari waliendelea na kazi yao ya kutibu wagonjwa. Shangaziye Alifurahia sababu Ali amebadilisha maisha ya wanakijiji. Ali aliota ndoto la kuwa mwananjeshi akikua mtu mzima. Alipenda sana.

5

Alipoamka alihadithia shangaziye ndoto hilo. Shangaziye Ali alimwambia kuwa hilo ni ndoto la kawaida na hakuamini. Ali alitaka sana kutimiza ndoto hilo na alipokua kijana mzima alianza kuenda mazoezi. Alifunzwa jinsi ya kulinda wanakijiji.

6

Ali alianza kuwapea ulinzi wanakijiji na shangaziye akiwa hapo pia. Mkononi alitumia mkuki na sime lenye makali. Alikua akiwalinda usiku na mchana. Alikua anaenda msituni kuwinda wanyama akiletea hao wanakijiji na shangaziye. Wanapika wote

7

Ali alitumia ngozi ya hao wanyama kutengenezea wanakijiji viatu,nguo,mipira na pia blanketi. Wanakijiji walifurahia sana na wote wakaishi kwa upamoja na amani. Wote walimpea Ali heshima sana na shangaziye akiwa mkuu wa kijiji hicho chote.

8
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
KIJANA MTIIFU
Author - Traccy Kairuthi
Illustration - Traccy Kairuthi, Simon Lewis
Language - Kiswahili
Level - First paragraphs