PUNDA MJINGA
Simon Lewis
Simon Lewis

Hapo zamani za kale kulikuwa na punda aliye kuwa akiishi msituni.Huyo punda alikua mjinga, kwa kuwa hakuwa akifikiria maamuzi anayo yafanya kabla na matokeo yatakuwa yapi. Wanyama pori wengine pia walikuwa wakiishi kwa huo msitu.

1

Simba alikuwa mfalme wao wakati ule .Simba alikuwa mfalme mwenye ukari sana .Alikuwa akiwanyanyasa wanyama pori wenzake.Siku moja kukawa kuna kiangazi .Ikawa hata Simba hangepata chakula chakutosha kwakuwa hata wanyama wengine waliangamia

2

Simba aliwezwa na akawa anakonda huku mifupa ikimtokea .Kwa bahati fisi alipokua akipita Simba alimuona na kumshauri amletee chakula na ikikosa yeye ndiye atakao kuwa chakula chake.Fisi alipatwa na wasiwasi sana aliodoka akiwa ameshtuka.

3

Alipokua akitembea alimpata yule punda.Alimsalimia punda kwa tabasamu na kumwaambia ana habari njema alikuwa akija kumletea.Punda alijiadaa kusikia huku akisikiza kwa makini. Fisi alimwambia punda kuwa Simba anataka kumfanya mfalme .

4

Punda alikuwa mwenye furaha tele alichukuwa hatua yakuenda kumwona Simba . Bila kuchelewa moja kwa moja hadi kwa mfalme wao Simba akiwa anatarajia kufanywa mfalme.Alipofika alimpata Simba pale na akamkaribisha.Punda akingoja awe mfalme.

5

Simba alijifanya kama ana mekelea mkono wake kwa ishara yakumachia ufalme na punda akaa vizuri akiwa ametulia .Ngafla simba aliyauma masikio ya punda.Punda aliruka kwa kilio akielekea kwa fisi iliameleze yalio tokea huko

6

Punda alimuwelezea jinsi Simba amemgoa masikio yake.Fisi naye kwa ujaja wake alimwambia punda"amekugoa masikio ili kofia lake lakiufalme likutoshee.",Alimshauri arudi tena huko ili afanywe mfalme.Kwa ile tabia yake yakutofikiria akarudi

7

Alipofika Simba alimgowa mkia wake nahuku punda akatoka kwa kilio .Fisi alimsikia pia akaenda tena nakupata mkia wake umegolewa alimwambia Simba alitaka aweze kuketi kwa kiti chake punda alirudi na Simba akaweza kumuangamiza akawa amefariki

8
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
PUNDA MJINGA
Author - Simon Lewis
Illustration - Simon Lewis
Language - Kiswahili
Level - First paragraphs