Ajabu ya wanyama
Mish Mish said
Salim Kasamba

Siku moja adhuhuri wanyama walifanya mkutano wenyewe ulihudhuriwa na wanyama wa kufugwa na wale wa porini pundamilia alisafisha koo kisha akawakaribisha wote waliofika "mkutano huo uliitishwa ili kujadili Uhuru wa wanyama ."

1

Ng'ombe aliomba kutoa maoni yake alitoa malalamishi yake dhidi ya binadamu alisema kuwalisha na kumpa maziwa mwanadamu kuna wakati angekosa kupewa chakula bora si hayo tu ng'ombe aliendelea kulalamika kuwa alilala sakafuni ambapo

2

Kumaja matope wakati mwingine angepigwa mijeledi alimwomba pundamilia kufikisha malalamishi yake kwa binadamu .Mbuzi na kondoo walisema walipitia shida Sawa na za ngombe .twiga alisema kuwa hakuwa na raha tena porini mahali pake pa

3

Malisho palijengwa hoteli mbalimbali za kifahari alilazimika kuhama kila ujenzi wa hoteli kama hizo ulipofanyika aliwauliza wanyama wenzake "je! mwanadamu akimaliza kujenga humu mwangu porini anatarajia Mimi nitaishi mjini kwenye ghorofa ?"

4

Pundamilia alimwona swara amejiinamia kwa huzuni akamuliza ndugu swara unaonekana kuhuzunika .nini chanzo cha huzuni yako swara alitikisa kichwa kama

5

ambaye alitaka mawazo yake kujipanga akilini alisema huzuni yake alitokana na namna yeye na swara wengine wanavyo windwa na mwanadamu alisikitika kuwa eti wanawindwa ndipo mwanadamu apate kitowea vilevile ngozi za swara zilihitajika

6

Kushonea mikoba na kutengenezea Ngoma pundamilia alisema wanyama wenzangu ni jukumu letu kuhudhuria na kujadili Uhuru wetu Kama tulivyofanya Leo nitafikisha ujumbe huu Kwa mwanadamu ni matumaini yangu kuwa akijua tumeanza kukutana atakoma .

7

Tena mnaoishi naye utawaweka katika mazingira safi mkutano ulimalizika na kila mnyama akarudi alikotoka .

8
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Ajabu ya wanyama
Author - Mish Mish said
Illustration - Salim Kasamba, Mish Mish said, Magriet Brink
Language - Kiswahili
Level - First paragraphs