Ngombe Wangu auzwa Kwa Bei nàfuu
Shalline Kadzo
Adonay Gebru

Siku moja baada ya ngombe wangu kununuliwa mama yangu aliniambia nenda ukalishe ngombe wako.Naenda sasa hivi mama.Baba alipoingia kutoka kazini alimkuta mama na mgeni mmoja anayeitwa Bwana Fadhili.Mgeni alimuuliza baba habari yautokako

1

Baba akasema Salama.Mama akasema huyu nimgeni anaitwa Bwana Fadhili amekuja Hapa kununuwa ngombe yule pale.Mama akaniita Kwa haraka Sana.Mama alinielezea kuwa ngombe wako ananunuliwa Sasa.Nilikasirika sana kusikia hivyo.Baba huyo

2

Naye hakupenda kwa sababu yule,aliyetaka kununuwa ngombe yule alikuwa nakiasi cha pesa cha elfu tano tu.Baba alikataa na yule bwana akaondoka taratibu nakwenda zake Mama ndiye aliye kasirika Sana,alitaka ngombe yule aliye wangu auzwe.Baba

3

alisema ngombe anatupa maziwa mengi sana kilasiku na kila asubuhi hunyui maziwa wewe mpaka unataka kuuza ngombe?".Mimi sikuwa nalakusema maana baba na mama walikasirikiana sana.Asubuhi niliamka nanjaa mno nilimkama ngombe wangu maziwa mengi

4

nanikayapika chai nyingi sana,kila mmoja alifurahia chai hiyo.Niliwaomba wazazi wangu waombane msamaha,baba alikubali kumsamehe mama.Mama naye alikubali kumsamehe baba.Yule bwana Fadhili akaja tena naakasema nitawaongezea pesa ili ninunuwe

5

ngombe yule,baba,mama,na Mimi tulikubali .Baba aliulizakiasi cha pesa pesa ngapi?Kiasi chapesa elfu ishirini tu baba alifurahi sana.Na bwana Fadhili akaondoka na yule ngombe.

6
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Ngombe Wangu auzwa Kwa Bei nàfuu
Author - Shalline Kadzo
Illustration - Adonay Gebru, Rob Owen, Jesse Breytenbach, Isaac Okwir
Language - Kiswahili
Level - First paragraphs