Safari ya mjini
Joy Kinya
Joy Kinya

Ilikuwa jumamosi moja ambayo mwalimu mkuu aliambia wanafunzi wote kuna safari ya kuelekea mjini. Wanafunzi wote walikuwa wamengoja kwa hamu na ghamu.

1

Kila mwanafunzi alijiandaa kwenda mjini. Siku ilipofika tulivaa sare rasmi za shule na kuondoka asubuhi na mapema.

2

Tulitumia basi la shule kuelekea. Tukiwa safarini tulitazama nje ya dirisha na tukaona matatu upande ule mwingine. Barabara za mjini zilikuwa zimestawika kweli kweli.

3

Kabla ya kufika mjini, tulipata magari yamesongamana barabarani kwa muda mrefu. Kawaida kwa barabara za vijijini haziko hivyo.

4

Kwa kuwa safari ilikuwa ndefu, dereva alitupa muda kidogo tushuke tuweze kupumzika kisha twendelee na safari.

5

Mara hivi tu tulivyorudi kwa basi na likasonga, tuliona lori kubwa limegonga gari ndogo. Tulijawa na wasiwasi kwani ilikuwa ajali barabarani. Ilisababisha msongamano wa magari kwa muda mrefu sana. Ilibidi tungoje.

6

Muda uliyoyoma na giza likaingia. Mwalimu alitwambia ni vizuri kulinda usalama unaposafiri kwa kufuatilia maagizo ya alama za barabara ili kuepukana na ajali. Safari yetu ilikomea hapo kisha tukaanza safari kurudi shuleni.

7

Tulihuzunika kwa kuwa hatukufika tulikokusudia.

8
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Safari ya mjini
Author - Joy Kinya
Illustration - Joy Kinya
Language - Kiswahili
Level - First paragraphs