Kwanini Mbuni Hana Manyoya Kwenye Shingo
Lewis Mutugi
Lewis Mutugi

Hapo zamani za kale paliishi Mbuni aliyependeza kweli kweli. Alikuwa na shingo ndefu yenye manyoya mazuri. Siku moja akiwa nyumbani kwake aliamua kwenda msituni kutafuta matunda.

1

Katikati ya msitu aliuona mti ambao ulikuwa na matunda. Alifurahi sana ingawa hakujua ule mti ulikuwa na mwenyewe ambaye ni joka mkubwa aliyeishi kando ya mti.

2

Alipokaribia ule mti nyoka yule alijitokeza. Mbuni alipomwona alijawa na hofu. Nyoka alimuuliza alichokuwa akitafuta. Mbuni alisema kuwa ana njaa na amekuja kutafuta matunda. Nyoka alisema kuwa yeye hapeani matunda yake. Mbuni alileta fujo.

3

Nyoka alimwambia Mbuni kuwa akimpa matunda naye ampe yai lake moja ambalo atataga. Mbuni alihuzunika na kukataa. Waliendelea kubishana.

4

Papo hapo walianza kupigana. Kwa ile harakati Nyoka alianza kummeza Mbuni. Alikasirika na kujivuruta ili kujiokoa mdomoni mwa Nyoka. Kwa bahati mbaya manyoya yaliyokuwa shingoni mwake yote yalitoka.

5

Alifurahi sana kunusurika kifo na alianza safari yake ya kurudi nyumbani huku akiwa na huzuni mingi sana kwani shingo yake ambayo iliyokuwa inapendeza ilibadilika na kuwa mbaya.

6

Barabarani alitimua mbio akihofia Nyoka anaweza kuwa anamfuata.

7

Tangu siku hiyo Mbuni alizoea kuishi bila manyoya shingoni, na wakawa maadui na Nyoka.

8
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Kwanini Mbuni Hana Manyoya Kwenye Shingo
Author - Lewis Mutugi
Illustration - Lewis Mutugi, Lewis Kinoti
Language - Kiswahili
Level - First paragraphs