

Hapo zamani za kale, kulikuwa na mzee aliyeitwa Joni. Joni alikuwa na mtoto wake Safir.
Joni na Safir walipendana na kufanya kila kitu pamoja. Safir alimheshimu babake sana.
Safir alikuwa mtiifu sana na alimsaidia babake kwa kufanya kazi za nyumba. Safir alikua akitoka shule, anaosha vyombo na kusafisha nyumba na pia kuhakikisha mambo yote yanasonga jinsi yanavyo faa.Alikua pia akiosha nguo zake.
Joni alitamani sana kuuza kofia.Akaoelea auze mfugo wake ili apate pesa ya kuanzisha shughuli hio ya kuuza kofia.Joni alienda akauza mfugo wake na akapata pesa za kununua kofia.Kisha akaenda na akanunua kofia za kuuza za aina mingi.
Mzee Joni alibeba mzigo huo akaingia kwa matatu na akaanza safari ya kurudi kwake.Katikati ya safari gari lilipata ajali lakini yeye hakukufa wala kupata jeraha lolote lile.Alitafuta gari lingine na likamfikisha nyumbani salama.
Mzee Joni alikaribishwa na kijana yake Safir kwa furaha tele. Safir alifurahia babake kua ataazisha biashara ya kuuza kofia. Alifurahia sababu ataweza kupata karo yake ya shule na pia wapate pesa ya kujikimu kimaisha na maitaji yao.
Mzee Joni alifika na kwanza kupumzika kwa safari hiyo. Alipomalizia alianza kutayarisha chakula cha jioni sababu masaa yalikua yamesonga kweli kweli. Alipika na kumaliza kisha wote wakaanza kukula kwa upamoja na walipomalizia kukula wakalal
Mzee alipokua amelala kijana yake Safir aliamka usiku na akaenda kuangalia hizo kofia. Akapata moja iko na picha kali ya kutisha. Alipiga duru kubwa ilyomamsha babake mbio. Akakimbia mpaka pahali mtoto wake alikuwa akiwa ameshtuka sana.
Kulipokucha mzee Joni aliamka na kuchukua kofia zake akaenda sokoni kuziuza na matarajio ya kupata pesa. Joni alifanikiwa kuuza na jioni akarudi na pesa mingi ajabu. Safir akalipiwa karo na zilizobakia wakanunua vyakula mingi sana vya kula.

