

Hapo zama za babu, palikuwa na msitu. Katika msitu huo, palipitia mto wa kipekee. Mto huu ulikuwa wa ajabu. Wanyama walioishi kwenye huo msitu walipenda kuutazama, lakini ilikuwa vingumu kufika karibu kwa kuwa msitu huo ulikuwa na malkia.
Miaka nenda miaka rudi, wanyama walijaribu kufikia msitu huo ingawa juhudi zao hazikufua dafu. Haja yao ilikuwa kuvuka ile ng'ambo ingine kwa kuwa upande wao ulikuwa mkavu.
Walitamani kula majani mabichi na kulala chini ya kivuli.
Siku moja malkia aliyekuwa anaishi mtoni kwenye msitu huo alifikiria kwenda kuwasaidia wanyama ambao waliokuwa pande hiyo iliyokuwa kavu. Alipanga safari yake kwa muda wa siku mbili.
Ala! Alishangazwa sana na mambo aliyoyaona. Alipata wanyama wengi wakifa kwa janga. Dunia yao ilikuwa kavu. Alikasirika sana na kugeuza rangi yake kuwa rangi ya kijani.
Malkia huyo alitandaa kwote, na kila alipopita paligeuka kuwa kama pande hiyo ingne ya mto. Nyasi ilimea na miti iliyokauka kurudisha uhai na kujawa na majani yaliyokuwa mabichi.
Wakati alipokamilisha kazi yake iliyomtuma pande hiyo alirudisha rangi yake ya kawaida iliyo kuwa hapo awali. Malkia huyu alifurahia sana na kungaa kama nyota kuelekea mtoni.
Alipofika mtoni pahali alipokuwa akiishi alipata makao yake yakiwa yametayarishwa na akaingia ndani ya maji na kuungana nayo kisha yakawa matulivu.
Siku moja wanyama walienda kwenye mto kunywa maji. Malkia alitokelezea kwa ghafla na kuwaambia wanywe maji na pia wao watang'aa kama majani mabichi.
Malkia alifurahi sana kujulikana na wanyama na kuwa hawakumwogopa tena. Waliishi maisha mema ya amani msituni.

