MZEE TAMAA
KENETH Mutwiri
Jacob Kono

Hapo zamani za kale katika Kijiji kimoja,aliishi MZEE aliyeitwa mzee Tamaa.

1

Mzee Tamaa alikuwa mwenye tamaa na ulafi. Alienda kila sherehe Kula na kunywa lakini hakushiba.Mara kwa mara mzee Tamaa aliketi na kujiuliza siku hiyo angela wapi.Alikumbuka kuna sherehe katika kijiji jirani.Alijipanga na kisha kuondoka.

2

Mzee Tamaa alikimbia ili asichelewe.Alipokuwa njiani alipatana na kijana mmoja.Kijana akamueleza kulikuwa na sherehe nyingine kwa mzee Juma.Mzee Tamaa akashindwa aende wapi.Aliamua kufika kwa kijiji jirani na kupata vyakula havijaandaliwa.

3

Alipoona hivyo akakimbia kwa juma na kupata pia hivyo bado havijapikwa.Mzee Tamaa aliskia vibaya sana.Alirudi kwa kijiji jirani na kupata vyakula vimeliwa na kuisha.

4

Bila kusita alirudi tena kwa Juma kwa haraka lakini alipofika alipata vyakula vivyokuwa vikiandaliwa pia vimeliwa na kuisha.Mzee alikasirika sana.Hapo ndipo alipojifunza kuwa mtaka yote hukosa yote.

5
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
MZEE TAMAA
Author - KENETH Mutwiri
Illustration - Jacob Kono
Language - Kiswahili
Level - First paragraphs