

Hapo zamani zakale,palikuweko na kidosho mmoja kwa Jina Mwanamize.Mwanamize alikuwa msichana mrembo mwenye madaha.Alikuwa na Pua ya kitara, kiuono cha nyigu na Shingo ya upanga.
Siku moja, wavyele wake Mwanamize waliondoka kwenda matembezini.wazazi wake Mwanamize walimwambia mwana wao kuwa hawakutaka atoke nje ya nyumba. Mwanamize aliwasikiliza wazazi wake kwa makini na kuwahakikishia kuwa angefuata maagizo.
Siku hiyo ,Rafiki zake Mwanamize walifika nyumbani kwa Mwanamize na kumwambia waende kutafuta kuni msituni. Mwanamize alijaribu kukataa lakini rafiki zake walimlazimisha aende nao.
Mwanamize aliandamana na marafiki zake kuelekea msituni.Walitafuta kuni hadi jua lilipokuwa likitua ndipo Mwanamize alipokumbuka kuwa alifaa kurudi nyumbani. waliharakisha kurudi nyumbani.
Walipofika Karibu na nyumbani Mwanamize alikumbuka alikuwa amesahau mkufu wake msituni. Mwanamize alirudi msituni Kuchukua mkufu wake uliopotea .Kabla ya Kuchukua mkufu wake Zimwi lililokuwalikitisha lilitokea.
Zimwi lilimchukua Mwanamize na kumtia Katika ngoma Zimwi lilienda Katika Kijiji cha akina Mwanamize ilikuwa likipiga ngoma Kwa kila nyumba Hulu Mwanamize akiimba. " NI MIMI MWANAMIZE MKUFU WANGU UKAGWA , ZIMWI LIKAJA LIKAMCHUKUA .
Bada ya kutembelea nyumba tatu alifika Katika nyumba ya akina Mwanamize. Alipokuwa akipiga ngoma Katika nyumba ya akina Mwanamize wazazi wake waligundua Kuwa Mwanamize ndiye Aliyevkuwa akiimba . wazazi wake waliimpa Zimwi chakula.
Walifungua ngoma na kumpata Mwanamize ndani ya ngoma.
Hapo ndipo Mwanamize aligundua kwamba ASIYESIKIA LA MKUU HUVUNJIKA GUU.

