Rose msichana mrembo
RAYMOND KALUME
Isaac Okwir

Hapo zamani za kale, katika kijiji cha Sombweto, palikuwa na msichana mrembo sana aliyefahamika kama Rose.

Rose alilelewa vyema. Alilelewa kwa tunu na tamasha kwani alikuwa ni mtoto wa pekee.

1

Alipotosha kuanza shule, alipelekwa katika shule nzuri sana iliyowavutia wazazi wake. Shule hii ilisifika sana kwa ubingwa wa walimu.

Kila mwaka watoto walikuwa wakipita mitihani yao vizuri na huwa na nidhamu ya hali ya juu.

2

Wazazi walioipata shule hiyo, walijiona wamebahatika sana. Wiki moja baadaye, Rose alianza kubadilika sana.

Alionekana akiwa kinyume na wenzake mwalimu alipokuwa akifundisha. Aliona ni kero kwake na kupigiwa makelele tu.

3

Mafunzo yote yaliingia sikio la kushoto na kutokea sikio la kulia. Alionekana akicheza darasani mara kwa
mara wakati mwalimu anafundisha.

Rose alizidi kubadilika kadri siku zinavyosonga. Siku moja Rose alionekana akiwa anasitasita.

4

Mwalimu alipomwuliza alisema alikuwa akiumwa na kichwa. Mwalimu alichukua hatamu na kuwaita wazazi wake.

Walipofika tu walimchukua hadi hospitalini. Walipofika huko vipimo havikuonyesha kitu chochote.

5

Baadaye Rose alirudi shuleni na kuendelea na masomo kama kawaida. Baadaye aliwaza na kuamua kutia bidii katika masomo yake.

Baadaye aliukalia mtihani wake wa kitaifa na kuufaulu vyema.

6
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Rose msichana mrembo
Author - RAYMOND KALUME
Illustration - Isaac Okwir, Jesse Breytenbach, Rob Owen
Language - Kiswahili
Level - Longer paragraphs