

Hapo Zamani za kale Wanyama wa porini waliishi mahali pamoja kama ndugu. Basi kwa Boma Mazima kuwe Na mzee wa Boma ili aongoze. Simba alichaguliwa awe kiongozi wa kupeana mashariti. Siku moja Simba aliwaambia waende Kutafuta chakula shamba.
Walipokua wakienda sungura aliwaambia watangulie yeye Yuko nyuma, kumbe ilikua no ujanja wake. Hakutaka kwenda. Wenzake walipoanza. Safari yeye alijificha kwa kichaka kandokando ya njia.Alikua akisubiri jioni akioona wenzake wakirudi awafua
Chui alimuona Yule sungura ujanja wake akaazimia moyoni mwake kwamba atahakikisha amemusema kwa Simba ili apewe adhabu. Aha walienda wakapata chakula chakutosha. Walikusanya mapochopocho ya know aina. Wakarudi nyumbani jioni.
Sungura alipowaona wenzake. Wakirudi alihisi moyoni mwake kua Chui. alimuona, kwa hivyo alimua kumuomba musamaha Chui ili asimushitaki kwa Simba. Walipo karibia mahali alipojificha alichipupa mbio Na wimbo wa kumusifu Chui. kama ifuatavyo,.
Chui ni mnyama mzuri Sana, anarangi nzuri Sana , mwendo wake wasitaha. Chui akasimama akamuuliza sungura, unanini nami? Mbona unanisifu hivyo? Sungura akamjibu ; Chanda chema huvishwa Pete kwa hivyo nione faragani nikupe uhondo.
Sungura akamwelezea Chui kua hakuenda Kutafuta chakula pamoja nao Na anahisi amemuona. Akaomba musamaha asimushitaki kwa Simba kiongozi wao. Chui akamuuliza atapata Nini kwa Murang'a hivyo. Sungura akamjibu atamsifu kwa Simba apewe cheo.
Hatimaye Chui alimusamehe sungura Na akapata tuzo la kua kiongozi.
Chui akawa akisikiza Na Wanyama site kushinda Simba.

