Ahadi ni deni
Ali Chai
Jacob Kono

Hapo Zamani paliishi mwindaji mmoja aliyekuwa maskini hohehae.Mwindaji Huyo alikuwa akiitwa Juma.Juma alikuwa mwindaji hodari Sana na alikuwa akiishi Na mkewe Sofia.Siku mmoja Juma alifunga safari kwenda msituni kuwawinda wanyama Na ndege.

1

Alimwaga mkewe na kuanza safari ya kwenda msituni.alipokuwa msituni akiwinda gafla akasikia Sauti mmoja ya kutisha Sana .Juma aliposikia Sauti hiyo alianza kutetemeka na kubwaga mkuki wake .Kufumba na Kufumba kulitokea Simba .

2

"kwanini unawaua wanyama hawa bila hatia yoyote",Simba alimuuliza Juma. Juma alimwelezea Simba mambo yote wanayo yapitia yeye pamoja na mkewe,na ataacha kuwinda endapo atakuwa tajiri. Simba alimwambia Juma kuwa angeweza kumpa utajiri .

3

Lakini Kwa sharti moja tu,endapo atarudi nyumbani na mtu yeyote aje amlaki inafaa aje ampe simba.Juma alikubali haraka Sana Na kumwahidi Simba .Simba huyo aliweza kutoweka Na kumwacha Juma akirudi nyumbani.

4

Juma alipofikia nyumbani hakuamini macho yake,alikuta jumba kubwa la kifahari na mifugo mingi ya kila aina pia kulikuwa na chakula kingi mno baada ya kufika mtoto wake wa kipekee alimkimbilia na kumlaki.Juma alipoona kuwa ni mwanawe,

5

Alihuzunika Sana mkewe alipomwona alijawa na wasiwasi wa mwasi aliyeasi kadamnasi ya insi.Alimwendea Juma,"kwanini una huzuni"Sofia alimuuliza Juma.Juma alimwelezea mambo yote,ndipo Sofia akamwambia Ahadi ni Deni Na inafaa uitimize.

6

Aliposikia alimbeba mwanawe na kumpelekea Simba.Simba alifurahi Sana.Juma alipokuwa akirudi ndipo alipokumbuka ahadi ni deni

7
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Ahadi ni deni
Author - Ali Chai
Illustration - Jacob Kono, Adonay Gebru
Language - Kiswahili
Level - Longer paragraphs