

Hapo zamani za kale kuliondokea banati mmoja aliyeitwa Jemima. Alijaliwa kukopolewa katika aila hohehahe ajabu.Kupika na kupakua ilikuwa shida mno.Uchochole uliwanuka kila waendapo.Licha ya uchochole huo,alibahatika kupelekwa Shule.
Yeye a likuwa kitinda Mumba.Alikuwa na kichwa chepesi na alifaulu katika mitihani yake.kila siku zilivyozidi kwenda ndivyo Maisha yalizidi kuwa magumu mithili ya ngarange za muvule.
Abu yake alipopiga aga dunia ilimulazimu asake vibarua vidogo vidogo.iliaweze kumusaidia Nina yake.Ilimbidi kuacha shule Kwa kipindi fulani.Hakujalilolote alijikazakisabuni.
Alijihimiza katika mitihani na hatimaye akamaliza darasa la nane .Matumaini ya kuendelea yalikuwa yamefifia kabisa.Ama kweli mcha Mungu si mfaki.Aliwezakupata mfadili na akayafadhili masomo yake.
Alimaliza masomo yake ya sekondari na hata ya chuo kikuu.Maisha ya aila yake yalibadilika.Uchochole haukuwa kilema kwa Jemimah.Aliwezakuwa peleka ndunguze shuleni.Sasa ndunguze wanafuraha lukuki.
Aila yake ilinawiri mithili ya waridi.sasa wanajulikana kama mabwenye wanaosaidia maskini.
Jemimah sasa hanabudi kumupa Mungu sukurani kochokocho.yeye Ni Mwalimu anayetajika Sasa.

