

Watoto watoto Mimi ninaitwa Kitosi Kibonde .Nimezaliwa huko Pemba .Sisi tunatokea familia ya kiislamu.Kwenye familia yetu tupo watu wanne.
Mama yangu anaitwa Zuwena Ali.Baba yangu anaitwa Mzee Kibonde Shomari.Nina mdogo wangu wa kiume aitwaye Ali.Ali ni mtundu kwelikweli.Leo nimepelekwa hospitalini ,ninauma sana.Ali yupo nyumbani angekuja hapa ingekuwa balaa yani mtoto hatulii
Wazazi wangu wanajituma sana ili niweze kufikia malengo yangu.Mimi kama msichana natakiwa kusoma kwa bidii ili nije kuwasaidia baadaye.Ninapenda sana kuwa Rais kama Rais
wetu Mama Samia.
Mama yangu hujishughulisha na kilimo na ufugaji.Yeye ni mwanamke shupavu sana.Kazi yake huingiza kipato kinachosaidia familia yetu.Pia tunapata maziwa na chakula ambacho huimaisha afya na ukuaji wetu.
Baba humsaidia sana mama kutimiza malengo yake na hata kwenye ulezi wa familia.Yeye anaduka la nguo .Baba anapokuwa nyumbani hutusaidia sana.Nashukuru Mungu kwa wazazi wangu.Watoto tuwaheshimu,tuwapende wazazi tufanikiwe katika maisha yetu

