NINAPENDA KUCHEZA
Nancy Kiama
Catherine Groenewald

Kiki: Habari Anna?

Anna: Njema Kiki. Umeshindaje?

Kiki: Nimeshinda vyema.

Anna: Njoo tucheze!

1

Kiki: Ndio tucheze mpira wa miguu.

Anna: Hapana, ningependa kucheza na baiskeli yangu mpya.

Kiki: Ndio! Tunaweza kucheza na baiskeli yako mpya.

2

Kiki: Iko wapi baiskeli yako Anna?

Anna: Ile pale chini ya mti.

Kiki: Baiskeli yako inapendeza!

Anna: Ndio tuliinunua na baba sokoni jana. Ninaipenda sana.

3

Kiki: Kalia nikusukume Anna.

Anna: Sawa, shika hapa niweze kukalia.

Kiki: Uko tayari nikusukume sasa?

Anna: Ndio, twende.

4

Anna: Asante Kiki kwa kunisukuma. Ungependa kuendesha baiskeli yangu mpya?

Kiki: Ndio Anna.

Anna: Basi njoo ukalie nikusukume pia.

Kiki: Asante Anna.

5

Kiki: Nimefurahia kucheza nawe.

Anna: Nami pia nimefurahia kucheza nawe. Kwaheri Kiki.

Kiki: Kwaheri Anna.

6
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
NINAPENDA KUCHEZA
Author - Nancy Kiama
Illustration - Catherine Groenewald
Language - Kiswahili
Level - First sentences