Msiba wa kujitakia hauna kilio.
Grace Mtawali
Kenneth Boyowa Okitikpi

Hapo zamani za kale,paliondokea familia moja iliyokuwa fukara sana.waliishi katika Kijiji kilicho itwa tabu. Kama jina la Kijiji chao,maisha ya Kijiji hicho yalikuwa ya kutapatapa.Lakini palikuwa na familia moja iliyojikaza kisabuni.

1

Familia hiyo ilikuwa na watoto watatu.watoto hao watutu ,wawili walikua watiifu na Yule mwingine hakusikia la mwadhini Wala la mteka maji msikitini.Alitia masikio take nta!.Wenzake waliendelea kusoma.

2

Japo maisha yao yalikuwa yakienda shaghalabagala lakini waliendelea kusoma kwa bidii.Baada ya muda mfupi ndugu yao alijiunga na genge la wezi.Wazazi wake walimuonya lakini hakuwasikiliza.

3

Hakutafakari chambilecho kuwa asiyefunzwa mamaye hufunzwa na ulimwengu.Kijana huyu alianza kuuza mihadarati.Baada ya siku chache pia yeye alianza kutumia.Siku moja Kama kawaida yake,alienda na kuuza madawa wa kukevya na genge lake.

4

Genge lake lilipenda kukaa katika vichochoro vya hapo kijijini ambako walifanya mambo yao and kufichicha polisi wasiwapate. Pakaja vijana wawili walionunua dawa za kulevya .

5

Aliwauzia mihadarati.Walipomaliza kula mihadarati hiyo walizimia ghafla binvu!.Kijana huyo hakujua mini cha ufanya.Alitapatapa jicho likamtoka.Kijasho chembamba kikaanza kumtoka na kutetemeka kama unyasi jangwani.

6

Pia jasho jekejeke likamtoka alishiwa na nguvu akawa Kama mtoto mchanga.Alijua ya kwamba siku yake yakula kalenda ilikua imefika.Alishikwa na kiwewe.Hapo kwa hapo wazo jinga likamjia la kutoroka mji huo na kuwaacha wali vijana wawili hapo.

7

Alipoondoka tu polisi wakaja na kuwakuta wale vijana.Wavulana walikuwa wamezimi. Waliwapeleka hospitalini.Madaktari walisema kuwa walikuwa wametumia mihadarati yenye sumu.Polisi waliwauliza maswali kama walikumbuka mtu aliyewauzia.

8

Nao wakasema ndiyo.Wacha polisi wamtafute kwa udi na usambara.Walisema endapo wangempata angejua kilicho mfanya kuku kukosa manyoya.Basi Kijana huyo akaanza kutafuta kwa udi na uvumba.

9

Baada ya siku tatu,alikamatwa na polisi wakiwa kwa msitu ulikwa karibu na Kijiji chao.Alifunguliwa mashitaka na kufungwa miaka kumi na tano gerezani. Alijutia kwa nini hakusikiza wazazi wake.

10
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Msiba wa kujitakia hauna kilio.
Author - Grace Mtawali
Illustration - Kenneth Boyowa Okitikpi, Jesse Breytenbach, Offei Tettey Eugene
Language - Kiswahili
Level - First paragraphs