Kisa ambacho sitakisahau
Grace Mtawali
Jesse Breytenbach

Siku ya likizo ya Disemba nilimtembelea nyanya yangu shambani. Nyanya alinikaribisha kwa furaha tele. Alinitolea chakula kitamu nikala mpaka nikamaliza.Nyanya alianzakunieleza Mambo mengi kuhusu shambani, maisha yake na majirani zake.

1

Nyanya alinieleza kuwa baba alipata posa ya kunioza.Ingwa hili halikuwa jambo geni kwangu kwa maana nilishawahi ona ndoa za mapema zikifanywa sikuwa tayari kuolewa. Nilikuwa nataka kusoma mpaka chuo kikuu. Jambo hili ilinitia hofu.

2

Sikujua nitapata msaada wapi.Nyanya aliniambia kwamba wageni watakuja siku ya jumatano na sikuruhusiwa kutoka inje hata kucheza na rafiki zangu. Pia sikuwa na njia ya kutoroka basi ili vunja matumaini yangu.

3

Siku zilizofuata, nyanya alinieleza Mambo ya uozo, ndoa na mtu atakaye nioa. Mimi nilikuwa na wasiwasi , mambo haya alikuwa magumu.Ilipofika siku ya jumatano nyanya aliniambia kwamba wangeni wangeingia saa tatu kasorobo hapo nyumbani.

4

Niliingia chumbani kwa nyanya yangu na niatulia tuli ilipofika saa tatu kasorobo nilisikia gari inaingia apo nyumbani nyanya alipofika ndani ya chumba chake alinipata nimeketi chini huku ninatetemeka Kama Jani la mgomba nyanya aliniambia

5

"Usiwe na wasiwasi kwa sababu ni hali ya kawaida" nyanya alitoka na wakaenda kwenye varanda ya nyumba.Walianza kusalimiana watu hao walikuwa wawili lakini mmoja ndiye alikuwa atakaye ozewa Mimi.Mtu huyo alikuwa anamwili mkubwa na tumbo.

6

Walianza kuzungumuza mambo yao ya Siri.Nilitenga sikio nikasikiliza mambo hayo yote waliyokuwa wakiongea.Baada ya mda walikuwa wamemaliza kuongea walielewana kumpatia pesa nyanya waje wanichukue siku iliyofuata. Nyanya aliwasindikiza inje.

7

Ni mda wakuondoka, msichana ambaye alikuwa na mimi alikwenda kuchukuwa afisa wa haki za watoto kwa ofisi za chifu. Alifika akanichukuwa wakati nyanya alikuwa inje. Kuko ofisini nilipata wasichana wawili waliokuwa walipangiwa kuozwa pia.

8

Afisa alipiga report kwa afisa was polisi, ambayo walienda kukamata wali watu waliokuja nyumbani. Mimi na wake wasichana wawill tulipelekwa kwa nyumba ya watoto.

9

Kisa hicho sitasahau Maishani mwangu. Kwa Sasa na fanya
bidii kwa masomo yangu, nifaulu maishani nisaidie watoto wengine wanaokaa katika Kijiji chetu.

10
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Kisa ambacho sitakisahau
Author - Grace Mtawali, Beatrice Kache, Amina Kazungu, Nuru Mramba
Illustration - Jesse Breytenbach, Wiehan de Jager, Brian Wambi, Adonay Gebru, Salim Kasamba, Rob Owen
Language - Kiswahili
Level - First paragraphs