

Hapo Zamani kuliishi msichana mmoja aliyeitwa Tausi.Tausi alikuwa msichana mzuri, alikuwa yuko katika shule us upili. Tausi alikuwa hana baba wala mama.Alitia bidii sana masomoni mwake.
Walimu wa shuleni mwao walikuwa wakimpenda sana Tausi.Tausi alikuwa Na marafiki wazuri,walikuwa wakimpenda sana.Siku moja, Tausi akaanza kushikana na marafiki wabaya.Walimu walimonya Ila Tausi hakusikia mawaidha yao. Alitaka kujivinjari nao
Tausi alikanza kusumbua darasa, mchezo mingi.Tausi alikuwa hafanyi vizuri wakipewa mtihani,Kwa sababu ya marafiki hao.Marafiki walianza kumshauri Tausi,kujiigiza Kwa mambo ya starehe na madawa ya kulevya
Sikh moja, Tausi alitoroka na marafiki zake wale wabaya,walienda matangani,basi marafiki wa Tausi walikuwa wavulana Kwa wasichana.Walipofika huko Tausi na wenzake walianza kula na kunywa madawa ya kulevya.Tausi alikuwa hajazoea kutumia.
Tausi alilala fofofo.Marafiki wake walimkimbia Tausi.Marafiki wengine wale wavulana walipomuona Tausi amelala walimfanya ngono.Tausi alipogutuka aliamka Kwa uharaka sana wavulana
wale walipomuona ameamuka walitoroka mbio za sungura.
Basi Tausi alibaki pale akiwa anajiuta, hakuweza kupiga repoti Kwa polisi au kusema Kwa walimu. Bada ya miezi miwili ilipopita Tausi alikuwa mjamzita. Hali yake ilikuwa yakusikitisha. Marafiki walimacha.Walimu yake walimuacha aendele kusoma
Tausi alijifungua mtoto wake kabla ya mtihani wakumaliza shule. Tausialiwaza na kuwazua, aligundua yakwamba asiye sikia la mkuu huvunjika guu.Maisha alikuwa magumu kwake.

