AJALI BARABARANI
Fatma Maleta
Rob Owen

Mama yao Hawa na Musa ni mgonjwa sana.Inawalazimu Musa na mdogo wake kwenda kumnunulia dawa.

1

Hawa na Musa wanatakiwa kuwa makini sana Barabarani kwasababu Kuna madereva wengine wazembe mno na uzembe wao husababisha ajali.

2

Wakati wakitembea barabarani , wanashudia ajali ya magari .Magari yanapoteza muelekeo

3

Magari Yale yanasabisha magari mengine yagongane .Hii ajali inasababisha maafa makubwa sana na watu wengi wanapoteza maisha na wengine kujeruhiwa.Uharibifu wa magari, majengo na biashara mkubwa unatokea

4

Majeruhi wanapelekwa hospitalini kwa gari la kubebea wagonjwa.Polisi nao wanawasili eneo la tukio.Tunapaswa kuwa makini wakati wowote barabarani.Kwaanzia watembea kwa miguu Hadi waendesha vyombo vya usafiri.Kuwa makini , okoa maisha.

5
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
AJALI BARABARANI
Author - Fatma Maleta
Illustration - Rob Owen
Language - Kiswahili
Level - First paragraphs