ZAWADI
Fatma Maleta
Brian Wambi

Zawadi ni mtoto mtundu sana.Anapenda sana michezo.Ni vizuri kucheza michezo salama ,na kuachana na michezo hatarishi.

1

Leo amecheza kombolela na kujificha kwenye mti .Baba na mama yake wamemshauri asicheze michezo hatarishi.

2

Wazazi wake wanampenda sana na kumuhamasisha acheze michezo salama.

3

Zawadi aliumia mguu wakati akishuka kwenye mti . Wazazi wake na watoto wenzake wanamliwaza asilie .Lakini Zawadi anashindwa kujizuia kulia kutokana na maumivu makali.

4

Zawadi ameacha kulia na kwenda kucheza na rafiki yake Tatu.Ameamua kuacha utundu na kucheza michezo salama.Baada ya kucheza wanarejea nyumbani akiwa na rafiki yake.

5

Zawadi na Tatu wanapokelewa kwa furaha sana .Leo ni siku ya kuzaliwa Zawadi na watu wote wanafuraha sana.

6
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
ZAWADI
Author - Fatma Maleta
Illustration - Brian Wambi
Language - English
Level - First paragraphs